Nyarugusu (Tanzania): mpango wa chakula PAM (WFP) uligawa maharagwe yasioweka kutumiwa na wakimbizi

Nyarugusu (Tanzania): mpango wa chakula PAM (WFP) uligawa maharagwe yasioweka kutumiwa na wakimbizi

Mwishoni mwa mwezi oktoba, PAM (mpango wa chakula duniani) ulitoa maharagwe ya viwango vibaya kwa wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu nchini Tanzania. Wakimbizi walitoa malalamiko kwa HCR na uongozi wa kambi hiyo. Kamati iliundwa ili kushughulikia tatizo hilo. Matokeo ni ya kustaajabisha ” maharagwe yaliotolewa hayawezi kutumiwa”. HABARI SOS Médias Burundi

Ni raia wenye asili ya Kongo waliokuwa wa kwanza kupewa maharagwe hayo yaliotolewa sambamba na mchele pamoja na mahindi. Jioni katika siku ya kugawa chakula hicho, familia zote zililalamika.

” Tumepewa maharagwe yasioweza kupikika”, wanalalamika.

Siku moja badaye, vyungu na sufuria zinazojaa “maharagwe” hayo zilipelekwa kwenye ofisi ya HCR na uongozi wa kambi. Hali ilitulia mara moja.

Wiki mbili badaye, zamu ya warundi iliingia lakini wao walikataa kupokea msaada huo.

” Tulikataa maharagwe hayo sababu hayawezi kutumiwa kama chakula” walibaini.

Mwishoni mwa novemba, kamati iliundwa. Inajumlisha mkuu wa kambi, wawakilishi wa wakimbizi, HCR, PAM pamoja na wizara ya mambo ya ndani ya Tanzania ambayo inahusika na wakimbizi na waomba hifadhi.

” Eneo lilitayarishwa vizuri na kuweka vyungu vikubwa vya cuma. Tulitumia miti mikubwa kama kuuni za kupika kilo 10 za maharagwe ndani ya chungu kimoja. Matokeo ni kwamba hakuna mbegu hata moja iliyowiva baada ya kupikwa kwa muda wa saa sita, waliarifu wajumbe wa kamati ambao waligundua kuwa maharagwe hayo hayawezi kutumiwa kama chakula.

PAM kulazimishwa kuyatoa katika ghala

Ikizingatiwa kiwango cha kuni ambacho anapewa kila mkimbizi, pamoja na muda unaotakiwa ili maharagwe hayo yaweze kupikwa, mnalazimishwa kubadili aina hiyo ya maharagwe na kuleta aina nyingine ya maharagwe mavuzi, na kuyaondoa mara moja katika ghala”, kamati iliamrisha shirika la PAM.

Kukataa kutii amri

Wiki tatu badaye, wakimbizi wanashuhudia kuwa maharagwe hayo bado yanasalia katika ghala. Wanangalia ghala hiyo asubuhi hadi jioni na wanahakikisha kuwa ” hakuna mfuko hata mmoja uliondolewa na tunahofia kuwa maharagwe hayo yakatolewa tena katika mgao ujao.

Wanaomba HCR na wizara ya mambo ya ndani ya Tanzania kuchukuwa hatua.

Kwa wakati huu, huenda mvutano umeanza kati ya wadau wa wakimbizi, upande mmoja mashirika ya misaada na serikali upande mwingine.

Mboga za majani ya viazi sukari kama njia mbadala

Wakati huo huo, ili kukidhi mahitaji ya chakula, wakimbizi wameamuru kula majani ya viazi sukari.

” Ni mara ya kwanza kwangu kutumia aina hiyo ya mboga. Lakini kwa sababu siwezi kutumia ugali wa mahindi peke yake, sina chaguo jingine. Kwanza kabisa mboga hizo zimeanza kuuzwa kwenye masoko kwa sasa”, anafafanua mkimbizi kutoka Burundi, baba wa watoto nane.

Zaidi ya wakimbizi 120 kutoka Burundi na Kongo wakaazi wa kambi ya Nyarugusu wanaomba taasisi husika ” kutafuta suluhisho la tatizo hilo linaloendelea”.

Previous Muyinga: moshi unaotokana na viripuzi vinavyotumiwa katika migodi ya dhahabu husababisha maradhi ya mapaafu na kifo
Next Meheba (Zambia): real community recovery for an estimated population of over 5,000 people