Minembwe: jeshi la Kongo na kundi la Twirwaneho walipoteza watu 11

Minembwe: jeshi la Kongo na kundi la Twirwaneho walipoteza watu 11

FARDC (jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo) na kundi la silaha la Twirwaneho walipigana siku ya alhamisi. Mapigano yalifanyika katika maeneo mbali mbali ya Minembwe, eneo linalokaliwa na wajumbe wa jamii ya Banyamulenge wengi wao wakiwa wafugaji. Eneo hilo linapatikana katika wilaya ya Fizi mkoa wa kivu-kusini mashariki mwa DRC. Jeshi lilipoteza watu saba wakati ambapo wapiganaji wanne wa kundi la waasi vijana Banyamulenge waliuwawa. HABARI SOS Médias Burundi

Mapigano yaliripotiwa katika maeneo ya Kabingo, Masha na Runundu.

Vyanzo maeneo hayo vinafahamisha kuwa jeshi la Kongo lilishambulia ngome za Twigwaneho kwa lengo la kuwasambaratisha.

” Vijana wa Twigwaneho walijihami vya kutosha dhidi ya shambulio hilo la ngome zake” vyanzo vya ndani vinasema.

Vyanzo katika jeshi vilihakikishia SOS Médias Burundi kuwa ” tulipoteza askali saba eneo la Minembwe wakati wa mapigano ya alhamisi”.
Viongozi wa kundi la Twirwaneho upande wawo wanatoa ushuhuda wao kwamba ” wanne kati ya wapiganaji wetu waliuwawa wakati wa mapambano dhidi ya FARDC”.

Kulingana na wazazi, kuna watoto wengi wa chini ya miaka nane waliojeruhiwa eneo la Runundu kutokana na mapigano hayo.

” ma mia ya watu walitoroka makaazi yao”.

Wanajeshi wa Burundi waliopiga kambi kivu-kusini chini ya himaya ya kikosi cha kanda ya EAC waliingilia kati ili kusaidia FARDC, vyanzo vya habari katika viongozi walifahamisha.

Maeneo yalichukuliwa

Wakati huo huo, jeshi la Kongo linahakikisha kuwa linadhibiti maeneo mengi yaliyokuwa katika mikono ya wapiganaji wa Twigwaneho eneo la Bijabo na vijiji vingi ndani ya wilaya ya Fizi.

Kundi hilo lilikuwa na ngome za kimkakati hususan eneo la Bijabo.

Jemedali Ramazani Fundi kamanda wa kikosi cha Sokola 2 anawaomba madiwani na wajumbe wa mashirika ya kiraia ya ndani kuwahamasisha wananchi ili waweze kushirikiana na jeshi la taifa kwa ajili ya kurejesha amani na usalama.

Previous Beni: waasi nane wa ADF wauwawa
Next Minembwe: the Congolese army and the Twirwaneho armed group have lost 11 elements