Beni: waasi nane wa ADF wauwawa

Beni: waasi nane wa ADF wauwawa

Jeshi la Kongo linafahamisha kuwa liliwauwa waasi nane na kuwakamata wengine 5 wa ADF (kundi la waasi wa Uganda) alhamisi hii katika kijiji cha Kisasu Ngandu. Ni katika wilaya ya Beni mkoa wa Kivu-kaskazini (mashariki mwa DRC). HABARI SOS Médias Burundi

Ni msemaji wa kikosi cha Sokola 1, kaskazini-kubwa aliyefahamisha hayo.

” Ni matokeo ya mapigano kati ya watu wetu na kundi la ADF katika usiku wa alhamisi kuamkia ijumaa kusini mwa eneo la Karuruma katika kijiji cha Bashi. Kwenye eneo la mapigano magaidi watatu wa ADF waliuwawa moja kwa moja. Miili mingine mitano ilipatikana baada ya mapigano”, aliripoti kepteni Antony Mualushayi.

Anazidi kuwa silaha aina ya AK-47 na vifaa vya mawasiliano vilikamatwa pia.

[…], baada ya kushindwa, aduwi alielekea katika mbuga ya wanyama ya Virunga. Tunawaomba raia wakaazi wa karibu na hifadhi hiyo ya kimataifa kuwa makini”, alizidi kusema.

” Kikundi cha ADF kwa sasa linakabiliwa na mashambulizi ya jeshi huku kikijaribu kulipiza kisasi wakati huu wa siku kuu. Huduma zetu maalum zilifichua mtandao wa magaidi wa ADF uliokuwa ikiandaa mashambulizi dhidi ya mji wa Béni “, alimalizia.

Previous Cibitoke: kilio cha raia waliofanyiwa mateso na kusikilizwa katika gereza la SNR mkoani
Next Minembwe: jeshi la Kongo na kundi la Twirwaneho walipoteza watu 11