Cibitoke: kilio cha raia waliofanyiwa mateso na kusikilizwa katika gereza la SNR mkoani

Cibitoke: kilio cha raia waliofanyiwa mateso na kusikilizwa katika gereza la SNR mkoani

Habari zilizokusanywa kutoka eneo hilo zinasema kuwa watu wawili wanafanyiwa mateso katika gereza la SNR (idara ya kitaifa ya ujasusi) mkoani Cibitoke (kaskazini-magharibi mwa Burundi). Hali hiyo ni kwa kipindi cha zaidi ya wiki moja. Wananchi na askali polisi wanafamisha kuwa wanawasikia wakiomba msaada. Viongozi wa SNR mkoani humo wanakanusha madai hayo. HABARI SOS Médias Burundi

Kulingana na vyanzo vyetu, wanaume hao wawili walifikishwa katika gereza hilo wiki moja iliyopita.

Kulingana na mashahidi, wafungwa hao wawili waliletwa na gari ya kiongozi wa idara ya ujasusi mkoani humo siku ya ijumaa tarehe 23 disemba wakitoka katika mkoa wa Bujumbura (magharibi) .

Wanatuhumiwa kushirikiana na kundi la silaha la waasi wa Burundi la Red-Tabara ” lililopiga kambi kivu-kusini (mashariki mwa DRC).

” wakati waliposimamishwa, alisema walikuwa na mpango wa kuvuka mpaka ili kujiunga na kundi hilo la silaha “, chanzo cha polisi kilifahamisha.

“Wanachapwa mara kwa mara ili wakubali kuwa wanashirikiana na kundi hilo la silaha linalopiga kambi nchini DRC kwa miaka mingi likipigana dhidi ya utawala wa Gitega”, polisi mmoja alibaini.

Askali polisi huyo anafahamisha kuwa wafungwa hao hawana haki ya kupata wageni na chakula.

Mawasiliano mengi kwa njia ya simu hufanyika kwa sasa kati ya viongozi wa idara ya ujasusi mkoani Bubanza ( jirani ya Cibitoke) na Cibitoke ili kuchukuwa maamuzi juu ya hatma ya watu hao. Muakilishi wa SNR mkoani Bubanza, Jovin Cishahayo anayefahamika zaidi juu ya vitendo vyake vya ukatili katika mikoa ya Makamba-Rutana (kusini-mashariki) pamoja na Gitega-Ruyigi ( mashariki na kati) ambapo alihudumu miaka ya nyuma.

” Tunahofia maisha yao. Watu wanaopita karibu na ofisi ya SNR mkoani Cibitoke huwa wanasikia kilio chao nyakati za usiku” , alifahamisha askali polisi mmoja.

Kulingana na yeye, ” wafungwa hao hawana hatia na wanazuiliwa kinyume cha sheria sababu hawakufanya kosa lolote”.

Anawatolea mwito watetezi wa haki za binadamu waweze kulazimisha wahusika ili watu hao waweze kuachiliwa huru sababu kulingana na matamshi yake, ” kama hakuna kitachofanyika haraka, hatari ya kufariki dunia katika jela la SNR mkoani Cibitoke iko juu sana”.

Akizungumzia mkasa huo, mkuu wa idara ya ujasusi mkoani Cibitoke Ahmed Nabil Sindayigaya anakanusha madai hayo na kufahamisha kuwa hakuna mtu hata mmoja anayezuiliwa katika idara ya ujasusi chini ya uongozi wake.

Aidha kuhusu utambulisho wa watu waliofungwa mikono na kusafirishwa siku ya ijumaa iliyopita usiku ndani ya gari ya idara ya ujasusi, aliamuru kusema bila kutoa maelezo mengi kwamba walikuwa wezi waliokamatwa katika tarafa ya Buganda (Cibitoke).

Previous Rwanda-DRC : spying accusations by the DRC presage an escalation of public incitement to violence
Next Beni: waasi nane wa ADF wauwawa

About author

You might also like

Governance

Rumonge: provincial authority is seeking aid for over 3,300 flood victims

On December 5, torrential rains hit localities in the commune and province of Rumonge (Southwest of Burundi). The local authorities gave a balance sheet of 3,370 needy people whose homes

Security

Kivu-kaskazini: Jeshi na kundi la M23 wanapigana eneo la Rutshuru karibu na RN2

Mapigano kati ya jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo na kundi la machi 23 yameshika kasi alhamisi hii 27 oktoba 2022 katika maeneo ya Chimirwa kwa takriban kilometa 4

Economy

Rumonge : intelligence seized a large quantity of fuel

This is a quantity of at least 2500 liters of fuel. The seizure took place in the Swahili neighborhood in the town center of the province of Rumonge (southwest Burundi).