Burundi: Floriane Irangabiye ahukumiwa miaka kumi jela

Burundi: Floriane Irangabiye ahukumiwa miaka kumi jela

Ni mahakama ya Mukaza katika jiji la Bujumbura iliyotoa hukumu hiyo. Floriane Irangabiye atalazimika kulipa faini ya milioni moja sarafu za Burundi. HABARI SOS Médias Burundi

Kesi hiyo imekatwa jumatatu hii, vyanzo karibu na faili hilo vimefahamisha SOS Médias Burundi.

” Amepatikana na kosa la usaliti na kushirikiana na makundi ya silaha” vyanzo vyetu vinasema.

Floriane Irangabiye alikabiliwa na mashtaka ya ” kuajiri wapiganaji wa kundi la Red-Tabara” , kundi la silaha la waasi wa Burundi lililopiga kambi katika mkoa wa kivu-kusini mashariki mwa DRC na kuchukuliwa na viongozi wa Burundi kama ” kundi la magaidi”.

Chanzo huru kilichopata nakala ya kesi kinathibitisha habari hizo.

” ili kuelezea juu hukumu hiyo, wamezingatia ripoti iliyotungwa na SNR ( idara ya ujasusi Burundi) na kuiga saini yake. Waliandika kuwa Floriane alikiri mashataka dhidi yake na kuomba msamaha. Lakini ni uongo ” , vyanzo katika idara ya sheria vinafahamisha.

Jumatatu, mshirika huyo wa radio ya ukimbizini ” Igicaniro ” na mawakili wake hawakuwa katika mahakama ya Mukaza ili kufahamishwa maamuzi.

Floriane Irangabiye aliripoti mahakamani tarehe 16 disemba iliyopita. Alitetewa na mawakili watatu ambao walitumwa na shirika la akinamama wanasheria.

Mtetezi huyo anayefanya harakati zake katika vuguvugu la akinamama na wasichana wanaotetea amani na usalama, alizaliwa nchini Rwanda na kuishi mjini Kigali tangu miaka saba iliyopita.

Alikamatwa wakati akielekea Burundi mwishoni mwa mwezi agosti 2022 kabla ya kuzuiliwa kwenye gereza la idara ya ujasusi katika jiji kuu la biashara la Bujumbura kwa siku nyingi.

Kwa sasa anazuiliwa katika gereza kuu la Muyinga ( kaskazini-mashariki mwa Burundi).

Mashirika mengi ya kiraia na yale ya kutetea haki za binadamu pamoja na wandishi wa habari walikosoa kifungo chake.

Wanataja kifungo hicho kama kinyume cha sheria na kuomba aachiliwe huru.

“Tunaomba sheria ichukuwe mkondo wake na kumuachilia huru sababu mashataka dhidi yake hayana msingi”, vyanzo karibu na faili hiyo vinafahamisha.

Mawakili wa mwanaharakati huyo tayari wamekata rufaa .

Previous Rutshuru: mapambano kati ya M23 na Maï-Maï
Next Kayanza: the price of the transport ticket is skyrocketing