Rutshuru: mapambano kati ya M23 na Maï-Maï

Rutshuru: mapambano kati ya M23 na Maï-Maï

Mapigano yameripotiwa siku ya jumatatu kati ya kundi la machi 23, M23 na Mai Mai. Mapigano hayo yalitokea kati ya Kisharu, kwenye umbali wa kilometa 30 ya makao makuu ya Kiwanja katika wilaya ya Rutshuru mkoa wa Kivu kaskazini mashariki mwa DRC. Wakaazi wengi wamekimbia maeneo yao kutokana na mapigano hayo. M23 inasema kuwa imejihami. HABARI SOS Médias Burundi

Vyanzo vya ndani eneo la Nyamilima vinafahamisha kuwa wakaazi wengi wa Kisharu walichukuwa muelekeo wa Kihito mashariki mwa kijiji chao.

Wengine waliamuru kujificha chini ya vitanda. Walichomoka baada ya kuondoka kwa waasi wa Mai-Mai.

Vyanzo vyetu vinahakikisha kuwa kundi la M23 ” linadhibiti kwa sasa eneo la Mirambi ambalo hadi jumatatu hii lilikuwa likichukuliwa kama eneo la kati kati “

Si mara ya kwanza kwa kundi la Mai-Mai na M23 kukabiliana katika eneo la Kisharu.

Mwishoni mwa novemba 2022 makundi hayo mawili yalipigana katika kijiji hicho na kusababisha hasara kubwa.

Baada ya kuchukuwa udhibiti wa vijiji vingine vitatu, mashirika ya kiraia ya eneo hilo yanatahadharisha juu kusonga mbele kwa kundi la M23 kuelekea eneo la Ishasha, linalopakana na nchi ya Uganda.

Mashirika hayo yanatuhumu waasi wa M23 kuiba ndani ya majumba wakati wakipita.

” Sisi hatuna desturi hiyo ya kuiba, kuuwa au kubaka wanawake. Hiyo ni mila ya FARDC na washirika wake”, alijibu gazeti la SOSMedias Burundi, msemaji wa kundi la M23 Canesius Munyarugero.

Bwana Munyarugero anakiri kuwa mapigano ” kati yake na FARDC na washirika wake kundi la Mai-Mai na FDLR” yalifanyika siku ya jumapili na jumatatu. Lakini alieleza kuwa M23 walijihami.

” Sisi, tunaendelea na kusitisha vita kama walivyotuomba wakuu wa nchi kupitia makubaliano ya Luanda (Angola) na Nairobi (Kenya). Lakini wanapotushambulia, tunalazimika kujihami na kuwarudisha nyuma. Hayo ndio yalitokea siku ya jumapili, alizidi kusema msemaji wa kundi la M23.

Canesius Karemera Munyarugero anasema ” ni uchochezi”.

Baadhi ya vyanzo kivu- kaskazini vimethibitisha vifo vya angalau wapiganaji nane wa kundi la M23 tangu jumapili iliyopita , habari zinazokanushwa na msemaji wa kundi hilo.

” Wanasema ni Rwanda iliyoshambulia. Ni wapiganaji gani hao waliouwawa ? Wanaweza kutoa utambulisho wao? alibaini Bwana Munyarugero.

Hali ya usalama mdogo mashariki mwa Kongo inaendelea kuwa chanzo cha mzozo kati ya Kongo na Rwanda, viongozi wa Kongo wakiendelea kukubaliana kuwa kundi hilo linaloundwa na raia wa kabila la watutsi linapata msaada kutoka Rwanda.

Katika hutba yake kwa taifa iliyotolewa jumamosi 31 disemba mjini Kigali, rais wa Rwanda Paul Kagame alituhumu jamii ya kimataifa kusifu na kutoa heshma kwa amani ya mdomoni na ” kuwapendelea viongozi wa Kongo kwa ajili ya kulinda maslahi yao”.

Kundi hilo la waasi wa kabila ya watutsi lililochukuwa tena silaha mwishoni mwa mwaka wa 2021, likituhumu viongozi wa Kongo kutotekeleza ahadi zake za kuwarejesha katika maisha ya kiraia wapiganaji wa kundi hilo, hivi karibuni liliachia sehemu ya ngome zake kikosi cha EAC, baada ya kutuhumiwa kuwauwa raia wa kawaida katika vijiji viwili chini ya udhibiti wa kundi hilo.

Kundi hilo lilikanusha madai hayo na kuomba uchunguzi huru ufanyike.

Kundi la M23 linadhibiti maeneo mengi katika kivu-kaskazini tangu mwishoni mwa juni iliyopita likiwemo eneo la Bunagana jiji la mpakani na Uganda.

Previous Burundi: Floriane Irangabiye sentenced to ten years in prison
Next Burundi: Floriane Irangabiye ahukumiwa miaka kumi jela