Tanzania: wakimbizi wa Burundi wanaomba mwaka huu uwe mwaka wa mateso kupungua

Tanzania: wakimbizi wa Burundi wanaomba mwaka huu uwe mwaka wa mateso kupungua

Mwaka wa 2022 wakimbizi wa Burundi wanaoishi katika kambi za Nyarugusu na Nduta wanasema kuwa walikabiliwa na changamoto nyingi na kuathiriwa na manyanyaso mengi. Wanaomba HCR na viongozi wa Tanzania pamoja na wadau wengine kuhakikisha mwaka huu unakuwa “mwaka wa unafuu”. HABARI SOS Médias Burundi

Kulingana na wakimbizi wa Burundi waliopewa hifadhi nchini Tanzania, mwaka wa 2022 ulikuwa ” mwaka mgumu kwetu”.

” Tulipata matatizo ya kiusalama, baadhi yetu waliuwawa, wengine kupotea na hadi sasa hawajulikani walipo, msaada wa chakula ulipungua vya kutosha, haki ya kupata matibabu imekuwa ngumu […], wanatakaja wakaazi wa kambi za Nyarugusuru na Nduta kaskazini magharibi mwa Tanzania.

Wakimbizi wengi wanakumbuka uharibifu wa vibanda na maduka ndani ya masoko ya ndani ya kambi.

” Ni njama za kutulazimisha kurudi Burundi”.

Viongozi wa kijamii wanadai kuwa hali ilianza kuwa mbaya tangu aprili wakati viongozi wa Tanzania waliamuru mashirika ya kiutu kupunguza misaada kwa wakimbizi wa Burundi kwa ” ajili ya kuwashawishi kurudi makwao kwa hiari “

” Sababu zilizotupelekea kutoroka bado zipo. Serikali ya Tanzania, HCR na washirika wake wangetakiwa kutusaidia kama inavyotakiwa kwa kuheshimu sheria zinazowahusu wakimbizi na waomba hifadhi “, wanatetea wawakilishi wa wakimbizi wa Burundi waliozungumza na SOSMedias Burundi.

Serikali ya Burundi ilituma wajumbe nchini Tanzania ili kuwahamasisha wakimbizi kurudi makwao. Wanadai kuwa ” hali ni tulivu ” ndani ya nchi na kwamba warundi wote wasiofuatiliwa na sheria wanatakiwa kurudi nchini kwa ajili ya kuchangia katika maendeleo ya nchi yao”.

” Hawataweza kamwe kutushawishi sababu tunafuatilia kinachoendelea katika nchi yetu. Kwanza tunashuhudia ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na unyanyasaji unaoripotiwa kila siku nchini Burundi sababu wakimbizi walitekwa na idara ya ujasusi ya Burundi kwa ushirikiano na zile za Tanzania. Baadhi hawakuonekana tena. Wengine walipelekwa jela nchini Burundi na hadi sasa hawajaachiliwa huru licha ya majaji kuwakuta hawana hatia baada ya kukosa ushahidi kuhusu tuhma dhidi yao kuhusu kushiriki katika makundi ya waasi”, walisema wakimbizi.

Hadi sasa, Tanzania ni nchi ya kwanza kutoa hifadhi ya ukimbizi kwa idadi kubwa ya warundi. Zaidi ya wakimbizi laki moja na elfu 45, idadi kubwa wakiwa walikimbia katika mwaka wa 2015 kutokana na mzozo wa muhula mwingine wa hayati rais Pierre Nkurunziza.

Ratiba ya kuwarejesha wakimbizi kwa hiari iliyoanza mwaka wa 2017 inaendelea huku kukiwa utashi mdogo kwa wakimbizi.

Mwishoni mwa mwezi novemba, wajumbe wa serikali katika kambi za Nduta na Nyarugusu walifahamisha kuwa nchi hiyo ndogo ya afrika mashariki ina mpango wa kuwarejesha zaidi ya wakimbizi elfu 70 katika mwaka wa 2023.

Previous Kivu-kaskazini: Kundi la M23 linadhibiti zaidi ya vijiji 100
Next Burundi: the president of the CNIDH renewed, activists in hope