Kivu-kaskazini: Kundi la M23 linadhibiti zaidi ya vijiji 100

Kivu-kaskazini: Kundi la M23 linadhibiti zaidi ya vijiji 100

Waasi wa kundi la machi 23 (M23) limechukuwa udhibiti wa jiji la kimkakati la Nyamilima, lilolo katika eneo la Binza tarafa ya Bwisha katika wilaya ya Rutshuru kwenye umbali wa kilometa 110 kaskazini ya mji wa Goma (makau makuu ya Kivu-kaskazini mashariki mwa DRC) kwenye umbali wa kilometa 20 kusini mwa mpaka na Uganda. Sehemu hiyo ilidhibitiwa jumatano asubuhi. Vyanzo katika utawala vinahakikisha kuwa kundi la M23 linadhibiti angalau vijiji 102. HABARI SOS Medias Burundi

Mashirika ya kiraia yanayotoa taarifa hizo yanafahamisha kuwa FARDC ( jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo) lilikuwa lilikimbia mji huo bila kutoa sababu siku nne kabla.

Eneo hilo lilikuwa chini ya udhibiti wa waasi wa Mai-Mai na washirika wao wa Nyatura kuanzia wakati huo ambao walikuwa wakionekana peke yao ndani ya mji huo na kulazimisha wananchi kutii amri zao , alithibitisha diwani mmoja .

Mji huo wa Nyamilima ulianguka katika udhibiti wa kundi la M23 baada ya hatua ya Kisharo.

Mbunge wa mkoa Alain Siwako anahakikisha kuwa zaidi ya vijiji 100 vya wilaya ya Rutshuru na vijiji vingine vya wilaya ya Masisi viko chini ya udhibiti wa M23 licha ya uwepo wa kikosi cha kikanda na Monusco ( Ujumbe wa umoja wa mataifa nchini DRC) na FARDC”.

Tukumbushe kuwa eneo la Binza katika wilaya ya Rutshuru linajumulisha vijiji zaidi ya kumi, kituo cha afya, kambi ya Monusco na vituo viwili vya mipakani na Uganda vya Ishasha na Munyaga, mbali na kuwa lango la kuingia katika wilaya ya Beni na Lubero kupitia ziwa Édouard.

Katika tangazo la tarehe 4 januari, kundi la M23 linafahamisha nia yake ya kuacha Rumangabo, eneo linalojumuisha kambi ya jeshi la FARDC na Kishishe/ Bambu alhamisi hii, ili kuchukuwa udhibiti wa maeneo mengine nyeti hususan Nyamilima na Ishasha ili kufuatilia vituo vya kuingia na kutoka nchini Uganda.

Kwa sasa, kundi hilo la waasi linalotajwa na serikali kama ” kundi la kigaidi” linadhibiti vijiji zaidi ya mia moja vya wilaya ya Rutshuru likiwemo eneo la makao makuu na kuendelea kuelekea eneo la Ishasha kwenye mpaka kati ya Uganda na DRC.

Hivi karibuni, kundi hilo la waasi la watutsi lililochukuwa tena silaha mwishoni mwa 2021 likiwatuhumu viongozi wa Kongo kutoheshimu ahadi zake kuhusu kuwarejesha katika maisha ya kawaida wapiganaji, liliacha sehemu ya ngome zake za Kibumba ( wilaya ya Nyiragongo) kwa kikosi cha kikanda. Baada ya kundi hilo kutuhumiwa mauwaji ya raia wa kawaida katika vijiji viwili chini ya udhibiti wa kundi hilo, linapinga madai hao na kuomba uchunguzi huru ufanyike.

Jumanne hii, msemaji wa kundi la M23 alifahamisha gazeti la SOSMedias Burundi kuwa ” tunachofanya ni kujihami dhidi ya mashambulizi ya muungano wa serikali.

Kupitia tangazo la jumatano hii, kundi la M23 linasalia na nia ya kutekeleza maazimio ya mikutano ya Luanda ( Angola ) na kutoa mchango wake katika juhudi za kikanda ili kupata amani nchini RDC.

kundi hilo linahakikisha hata hivyo kuwa ” linaendelea kujihami na kuwalinda wananchi katika maeneo chini ya udhibiti wake.

Previous Tanzania: Burundian refugees plead for a better year
Next Tanzania: wakimbizi wa Burundi wanaomba mwaka huu uwe mwaka wa mateso kupungua