Burundi-RDC : Burundi inatuma kwa mara nyingine wanajeshi nchini Kongo

Burundi-RDC : Burundi inatuma kwa mara nyingine wanajeshi nchini Kongo

Kwa mjibu wa katibu wa kudumu wa baraza la kitaifa la usalama, kundi la pili la wanajeshi wa burundi limewasili kwenye ardhi ya kongo jumatano hii. Wakati ambapo kikosi cha kwanza kilichoingia DRC kinaendesha opereshini chini ya mwamvuli wa ushirikiano, hichi kikosi cha pili kitakuwa chini ya amri za kikosi cha kikanda kilichoamuliwa na wakuu wa nchi za EAC mwishoni mwa mwezi juni. HABARI YA SOS Medias Burundi

Kanali Pierre Claver alifahamisha hayo jumanne jioni katika mkutano kuhusu hali ya usalama nchini.Mkutano huo ulifanyika mkoani Rumonge kusini magharibi mwa nchi.

“Tutatuma vikosi viwili nchini Kongo. Cha kwanza kiliombwa na Kongo yenyewe katika hali ya ushirikiano wa nchi hizi mbili.Kikosi cha pili kitatumwa kesho (jumatano) chini ya mwamvuli wa kikosi cha kikanda cha EAC. Vyote hivyo vitashirikiana lengo likiwa moja:” kurejesha amani mashariki mwa Kongo” alisema hayo kanali Nzisabira .

Na kuzidi : “Mnapo jiweka kati ya ndugu wawili wanaopigana, aidha mnajeruhiwa au mnakufa.Watu wanatakiwa kuelewa hilo.”

Frédéric Bamvuginyumvira aliyewahi kuwa makamu wa rais wa Burundi, mtazamo wake ni kwamba ni jambo lisiloeleweka kwa nchi ambayo haina uwezo wa kulipa michango yake katika mashirika ya kikanda na kimataifa kuweza “kupata pesa ya kuwahudumia wanajeshi wake walio nje ya ardhi yake.” anasema

Viongozi wa Burundi wanahofia kisasi. Karibu wa kudumu wa baraza la usalama alitahadharisha wamiliki wa ma hoteli na nyuma za kupokea wageni. Anafikiri kuwa “waasi watashindwa kwenye uwanja wa mapambano” na hivyo kuwasili nchini Burundi kupitia ziwa Tanganyika na kuleta silaha na kuvuruga usalama na kufanya maajabu iwapo wataweza.”

Idadi ya askali jeshi wa Burundi waliopokelewa jumatano hii katika mkoa wa Kivu ya kusini haikujulikana.Vyanzo mjini Uvira na katika bonde la Rusizi wameambia chumba chetu cha habari kuwa wameshuhudia viongozi wa jeshi la Kongo wakijiandaa kwenda kuwapokea wanajeshi wa FDNB (jeshi la Burundi) .

Lakini jeshi la FARDC (Jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo) na FDNB wamethibitisha kuwa idadi ya wanajeshi wa kikosi kilichotumwa mwezi agosti ni kati 600 na 630.

Hadi sasa, nchi nne kwa jumla ya saba za jumuiya ya kiuchumi ya afrika mashariki ndio tayari walituma wanajeshi nchini Kongo. Nchi hizo ni pamoja na Uganda na Burundi zilizosaini makubaliano ya ushirikiano na DRC, Tanzania ikiwakilishwa kijeshi katika kikosi cha umoja wa mataifa Monusco (ujumbe wa umoja wa mataifa nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya kongo) ambacho kinalaumiwa sana na wananchi wanaoshutumu kikosi hicho kutowajibika pamoja pia na Kenya.
Mikoa inayohusishwa katika opereshini ya kikosi hicho cha kikanda ni pamoja na Kivu kaskazini, Kivu ya kusini na Ituri.

Makubaliano ya hivi karibuni ya Nairobi kati ya serikali ya Kongo na makundi ya waasi hayakumaliza tatizo ya usalama mdogo katika eneo hilo la Kongo lenye utajiri mkubwa wa madini.

Previous Burundi-DRC : Burundi sends other soldiers to Congo
Next DRC (Beni) : Shambulio jingine la waasi wa ADF limewauwa makumi ya watu eneo la Banande-Kainama