Tanzania : zaidi ya wakimbizi 4750 wa burundi wamekamatwa kwa kipindi cha miezi minne wakijaribu kwenda katika za ukanda huu

Tanzania : zaidi ya wakimbizi 4750 wa burundi wamekamatwa kwa kipindi cha miezi minne wakijaribu kwenda katika za ukanda huu

Takwimu hizo zilitolewa na huduma ya uhamiaji katika tarafa ya Kakonko, kanda ya kigoma (kaskazini-magharibi mwa Tanzania) ambako wahusika wanapitia. Ilikuwa alhamisi hii. Kulingana na ushuhuda wa wakimbizi, wanataka kukimbia kambi nchini Tanzania kutokana na hali mbaya ya maisha. Hakika ni karibu 4750 wanaohusishwa. HABARI ya SOS Medias Burundi

Kulingana na viongozi nchini Tanzania, ni wakuu wa familia changa pamoja na wale wanaowategemea ambao kubwa wanakamatwa katika visa vingi.

” Ni rahisi kwao kutumia usafiri wa watu na vitu ukilinganisha na takaba zingine za wakimbizi. Na hilo kwa safari ndefu” vyanzo vyetu zinadai.

Wakimbizi wa burundi waliokamatwa walitaka kuelekea nchini Rwanda, Uganda, na Kenya kwa mjibu wa huduma ya uhamiaji eneo la Kakonko.

” Tunakabiliana na hali ngumu ya maisha ndani ya kambi.Msaada wa chakula hautoshi na shughuzi za kuleta faida zilisimamishwa. Tunapata pia ugumu kutoka ili kwenda kulima katika mashamba ya watanzania au katika vijiji vya karibu. Hali inaendelea kuwa ngumu kwetu ndio maana tunataka kwenda sehemu nyingine. Cha ajabu ni kwamba wanataka kuturejesha nyumbani kwa nguvu “, wamefafanua kwa polisi ya tanzania warundi waliokamatwa eneo la Kakonko.

Kakonko tarafa ambako kunapatikana kambi ya Mtendeli iliyofungwa hivi karibuni inasalia eneo peke la mpaka ambako warundi wanaokimbia kambi huwa wanalazimika kupita ili kuwasiki katika nchi za kanda hii wanakotaka kufika.

Kwa mjibu wa wandishi wetu ndani ya kambi za wakimbizi wa burundi nchini Tanzania, wakimbizi kwa sasa hawaripoti kwa wingi zoezi la kurejeshsa nchini kwa hiari katika miezi ya nyuma. Hali hii inawapelekea viongozi wa Tanzania kudumaza hali ya maisha ndani ya kambi.

Tanzania inasalia kuwa nchini ya kwanza inayopokea wakimbizi kutoka burundi. Inawapa hifadhi takriban laki moja na elfu 27 ambao wako katika kambi mbili ambazo ni Nduta na Nyarugusu katika mkoa wa Kigoma kaskazini-magharibi mwa nchi.

Previous Burundi-RDC : Burundi inatuma kwa mara nyingine wanajeshi nchini Kongo
Next Cibitoke : Zaidi ya familia 100 walifukuzwa nje ya ardhi zao eneo la Rugombo