Cibitoke : Zaidi ya familia 100 walifukuzwa nje ya ardhi zao eneo la Rugombo

Cibitoke : Zaidi ya familia 100 walifukuzwa nje ya ardhi zao eneo la Rugombo

Karibu familia mia moja kwenye kitongoji cha Mbaza-Miduha kijiji cha Rukana ya pili tarafani Rugombo katika mkoa wa Cibitoke (kaskazini-magharibi mwa Burundi) wanasema kuwa walinyanganywa ardhi zao. Wanawanyoshea kidole na kuwatuhumu viongozi tawala katika mkoa huo kuwa waliahidi kupatia ardhi hizo vigogo wafuasi wa chama cha CNDD-FDD. Gavana wa mkoa anakiri ardhi hizo ni miliki ya a serikali. HABARI ya SOS Medias Burundi

Takriban familia 110 zilizokuwa kwenye ardhi yenye ukubwa wa heka 80 wamefurushwa nje ya ardhi yao kwenye kitongoji cha Mbaza-Miduha.

Kulingana na vyanzo vya habari sehemu hiyo, vijana Imbonerakure ( wafuasi wa chama tawala cha CNDD-FDD) walimiminika wakiwa idadi kubwa tangu wiki moja na kuwalazimisha jumla ya wakaazi wa eneo hilo kuondoka mara moja bila masharti.

“Vijana hao walituambia kuwa tunaishi katika ardhi zinazomilikiwa na serikali na kwamba hatuna haki yoyote za kuendelea tukiishi eneo hilo” ameeleza mkaazi mmoja aliyekutwa sehemu hiyo.

Kulingana na wakaazi, ” ni hali ya kupokonywa ardhi kwa manfaa ya ummaa. Ardhi hiyo zimechukuliwa na kupewa vigogo raia na wanajeshi wafuasi wa chama cha CNDD-FDD”.

Chanzo katika watu wakuu kinafahamisha kuwa zaidi ya heka 100 za ardhi eneo hilo zilikabidhiwa watu wa karibu na CNDD-FDD mwanzoni mwa mwaka huu.

Baadhi ya wakaazi wa Mbaza-Miduha wanaishi eneo hilo kwa zaidi ya karne moja.Wengine walikabidhiwa ardhi kisheria na wako na karatasi za umuliki wa ardhi. Familia zilizopokonywa ardhi hizo upande wao wanawaomba viongozi wanaohusika “Kuheshimisha haki yao kwenye ardhi za ma babu zao”.

Gavana wa mkoa wa Cibitoke anakiri kuwa ardhi hiyo ya Mbaza-Miduha ni mali ya serikali na kwamba serikali inachukuwa mali yake. Ama kuhusu swali kwamba ardhi hizo zinakabidhiwa kwa watu wa karibu na chama tawala na kwa baadhi ya wafanyakazi wa ummaa baada ya kunyanganywa wakaazi, Carême Bizoza amejizua kusema lolote.

Previous Tanzania : zaidi ya wakimbizi 4750 wa burundi wamekamatwa kwa kipindi cha miezi minne wakijaribu kwenda katika za ukanda huu
Next Tanzania : nearly 4,750 Burundian refugees arrested trying to reach other countries in the region in four months