Bubanza : visa zaidi ya 140 vya Covid-19 vyapatikana katika gereza la mkoa

Bubanza : visa zaidi ya 140 vya Covid-19 vyapatikana katika gereza la mkoa

Zaidi ya wafungwa 140 walipatikana na virusi vya Covid-19 ndani ya gereza kuu la mkoa wa Bubanza (magharibi mwa Burundi). Wengi kati yao walipona baada ya kupokea huduma za matibabu. Angalau kumi waliopatikana na maradhi hayo waliwekwa karantini wakisubiri wapone. HABARI SOS Médias Burundi

Kulingana na vyanzo katika gereza la Bubanza, mfungwa asiyekuwa na virusi ya Corona ni yule ambaye ana uhusiano na watu wa nje peke.

Kwa kipindi cha wiki moja, wafungwa 143 waliambulizwa ugonjwa huo kwa jumla ya wafungwa 500.

Viongozi wa magereza pamoja na afya katika mkoa wa Bubanza walitahadharishwa na kuchukuwa hatua za kudhibiti maambukizi ya virusi hivyo . Zoezi la kuwapima wafungwa wote kilifanyika ” chanzo cha karibu na jela la Bubanza kilifahamisha.

Wagonjwa wanne mahtuti walipelekwa kwenye hospitali ya mkoa. Wanapewa huduma za dhadura katika kituo hicho cha afya.

“Wote walipona na walirudishwa ndani ya gereza”, vyanzo vyetu vilithibitisha.

Hatua kwa ajili ya kudhibiti maambukizi

Mara baada ya kugundulika kisa cha kwanza, wahudumu wa afya walifanya kampeni ya kupima ugonjwa huo . Harafu walinyunyuzia dawa mahala ambapo wafungwa wanalala. Wagonjwa waliwekwa pembeni ili kuepusha kuambukiza wafungwa wote na kuwazuia kukutana na wageni kutoka nje ya gereza.

” Tunajipongeza kuwa hatua hizo zilileta matunda mazuri. Upande wa akinamama visa viwili tu ndivyo vinasalia” , vyanzo vyetu vilifahamisha.

Katika mkoa wa Bubanza nje ya gereza, hakuna hatua ya kukataza watu kusogeana iliyochukuliwa katika maeneo ya mikusanyiko kama soko, kanisa na katika mikutano. Hakuna kuvaa barakoa au kuweka ndoo kwa ajili ya kunawa mikono.

Na gerezani, uangalifu ni mkubwa, wagonjwa waliopona wanasalia chini ya uangalizi wa waganga.

Nje ya gereza, idadi ya waliopatikana na Covid-19 bado kujulikana.

Katika kipindi cha wiki moja peke, angalau watu 439 walipatikana na virusi hivyo ndani ya nchi hiyo ndogo ya afrika mashariki kwa mjibu wa SOS Médias Burundi.

Previous Burundi : chama cha CNDD-FDD chajijenga upya pasina mpasuko
Next Rwanda : Congolese refugees refer to embassies in Kigali