Burundi : chama cha CNDD-FDD chajijenga upya pasina mpasuko

Burundi : chama cha CNDD-FDD chajijenga upya pasina mpasuko

Chama cha CNDD-FDD kiliandaa jumapili hii kongamano katika jiji la kisiasa la Gitega. Idadi kubwa ya waangalizi walitaraji kuwa watatofautiana. Lakini chama tawala kilitangaza baadhi ya mabadiliko pasina mpasuko kama walivyotaraji baadhi. HABARI SOS Médias Burundi

Kongamano hilo lilisubiriwa kwa hamu kubwa. Hata waziri wa mambo ya nje alichukuwa jukumu la kuwaalika wanadiplomasia wanaofanyia kazi nchini Burundi ili waweze kuelekea katika mji mkuu wa kisiasa wa Gitega. Wana makaazi katika jiji la kibiashara la Bujumbura kwenye umbali wa kilometa zaidi ya 100. Idadi kubwa waliitikia mwaliko. Hao ni pamoja na wawakilishi wa mabalozi wa marekani, uholanzi, uturuki, China na Tanzania….

Baada ya maombi yaliyojumulisha dini zote na hutba ya uzinduzi ya rais wa nchi, wajumbe wa chama cha CNDD-FDD kutoka mikoa 18 ya nchi hiyo ndogo ya afrika mashariki, walikutana faraghani. Baada ya takriban saa moja, Nancy Ninette Mutoni, afisa wa chama anayehusika na mawasiliano alisoma tangazo la kukamilisha shughuli za kongamano hilo.

Alitangaza mabadiliko mengi: uundwaji wa taasisi za chama ndani ya vijiji, mabadiliko katika taasisi za chama kwenye ngazi ya mikoa, uundwaji wa taasisi mbili mpya zitakazohusika na shughuli na programu za wapiganaji wa zamani wa kundi la zamani la waasi wa kabila la wahutu.

Révérien Ndikuriyo alichaguliwa kwa utulivu kuendela na uongozi

wawakilishi wa CNDD-FDD walijieleza pia kuhusu uhusiano kati ya Burundi na nchi zingine, hususan Rwanda.

[…], Chama cha CNDD-FDD kinaomba Rwanda kukabidhi nchi ya Burundi watuhumiwa wa jaribio la mapinduzi wanaokimbilia katika nchi hiyo tangu 2015, na wahalifu wengine 19 wa Burundi waliokimbilia kwenye ardhi ya Rwanda baada ya kufanya mashambulizi dhidi ya Burundi mwezi septemba”. Ni baadhi ya mapendekezo ili uhusiano kati ya nchi hizo mbili za maziwa makuu ya afrika ” uweze kuimarika daima”.

Chama tawala kinahakikisha kutambua juhudi za Rwanda za ” kuwaacha wakimbizi wa Burundi warudi makwao” na kuitaka nchi hiyo kuendelea katika njia hiyo.

Tangazo hilo la kuhitimisha kongamano la kundi hilo zamani la waasi wa kihutu liliwashahuri raia wa Kongo” kusimamisha kwa pamoja ili kuipesha nchi hiyo kusalia katika vurugu”.

Rais wa Burundi aliyechukuwa takriban masaa mawili ya kuzungumza, alirejelea washirika wake wanaokula rushwa na wasiokuwa na maadili.

” viongozi wanaokula rushwa wanatakiwa kuelewa kuwa nyakazi hizo zimepitwa na muda. Tulichaguliwa ili tuwahudumie wananchi na sio kuwatesa na kuhodhi mali zao. Tunalipwa pesa kutoka kodi na ushuru kutoka kwa wananchi lakini munawaomba rushwa kabla ya kuwahudumia”, alizidi kushambulia bwana Ndayishimiye anayewataja viongozi hao kama wahalifu”.

Hatua nyingi za usalama zilichukuliwa wakati wa kongamano hilo la jumapili na hakuna hata mtu mmoja aliyeruhusiwa kuingia eneo la kongamano akiwa na simu ya mkononi.

Kabla ya kongamano kufanyika, chama tawala kiliandaa maombi ya siku tatu. Askofu mkuu wa Gitega aliyezindua maombi hayo aliwaomba viongozi kutoka chama cha CNDD-FDD na wawakilishi wa chama hicho, ” kuimarisha uheshimishwaji wa haki za binadamu”.

Previous Photo of the week : the Archbishop of Gitega calls on the CNDD-FDD and Burundian authorities to promote the respect for human rights
Next Bubanza : visa zaidi ya 140 vya Covid-19 vyapatikana katika gereza la mkoa