Rwanda-DRC : jeshi la Rwanda limeshambulia ndege ya kivita ya Kongo
Rwanda inathibitisha kuwa ” imechukuwa hatua za kujilinda na kushambulia ndege ya kivita ya Kongo inayokiuka jumanne hii tarehe 24 januari anga ya Rwanda”. Ni mkasa wa tatu wa aina hiyo uliyoripotiwa na viongozi wa Rwanda tangu novemba 2022. HABARI SOS Médias Burundi
Kwa mjibu wa tangazo la serikali ya Rwanda lililopitishwa kwenye ukurasa wa Twitter, tukio hilo limejiri saa 10:03 alasiri. Serikali ya Rwanda inasema ni uchokozi na kuomba DRC kuachana na aina hiyo ya uvamizi”. Anuani rasmi ya mkoa wa Kivu-kaskazini mashariki mwa Kongo kwenye mpaka na Rwanda, inahakikisha shambulio hilo.
” Ndege haikuguswa, ilijihami kwa kutumia mfumo wake dhidi ya makombora na ni mioto mulioona na moto huo umeteketeza bomu lililorushwa na Rwanda”. imesomeka kwenye anuani hiyo.
Tangu novemba 2022, ni mara ya tatu kwa viongozi wa Rwanda kudai kuwa anga yake imeingiliwa na ndege ya kivita ya Kongo. Kisa cha hivi karibuni ni cha mwishoni mwa disemba.
Tarehe 29 disemba iliyopita, Rwanda ilituhumu jeshi la Kongo kuvamia anga yake, madai yaliyopingwa na viongozi wa Kongo kupitia tangazo.
Uhusiano kati ya mataifa hayo mawili ya maziwa makuu unazidi kuzorota tangu kundi la machi 23, M23 kuanzisha mashambulizi tena.
Kundi hilo la waasi la watutsi lilichukuwa silaha tena mwishoni mwa mwaka wa 2021 likituhumu viongozi wa Kongo kushindwa kutekeleza ahadi zake kuhusu kurejesha wapiganaji wake sehemu kubwa wakiwa watutsi wa Kongo katika maisha ya kawaida.
Viongozi wa Kongo wanaendelea kukubaliana kuwa kundi hilo linaungwa mkono na Rwanda, madai ambayo serikali wa Rwanda inazidi kukanusha na kutupilia mbali.
Rais wa Rwanda Paul Kagame alituhumu mara kwa mara jamii ya kimataifa ” kupendelea viongozi wa Kongo na kusifia amani ya mdomoni” nyakati zilizopita.
You might also like
Rwanda-DRC: the Rwandan army announces that it has repelled an aggression by Congolese soldiers
The incident took place this Wednesday around 4:30 a.m, a press release from the Rwandan army says. It took place between the district of Rusizi in the western province of
Giharo : attempted arrest of a district leader of the UPRONA party
Usuel Ntakarutimana, leader of the UPRONA party (Union for National Progress) in Giharo district in Rutana province, southeast Burundi, was the victim of an attempted arrest by the district leader
North Kivu : the M23 has once again recovered Kishishe
M23 rebels have once again seized Kishishe, a village located in the North Kivu province in eastern DRC. A year ago, the Congolese authorities accused the rebellion of having killed
