Rwanda : zaidi ya wakimbizi wapya 3000 kutoka Kongo wapokelewa

Rwanda : zaidi ya wakimbizi wapya 3000 kutoka Kongo wapokelewa

HCR inafahamisha kuwa inaendelea kuwapokea wakimbizi kutoka Kongo wanaokimbilia nchini Rwanda. Zaidi ya wale 3000 tayari waliwasili wiki chache zilizopita. Kituo kipya cha muda kiliandaliwa eneo la Nkamira karibu na mpaka wa Kongo kwa ajili ya kuwapokea wakimbizi hao kutoka kongo,idadi kubwa wakiwa watumiaji wa lugha ya Kinyarwanda. HABARI SOS Médias Burundi

Shirika hilo la umoja wa mataifa linafahamisha kuwa raia wa Kongo wanaotoroka mapigano mashariki mwa DRC wanaingia kwa wingi nchini Rwanda.

“Karibu wapya 3000 wanaotoka nchini DRC walikimbilia nchini Rwanda wiki chache zilizopita. Pamoja na serikali ya Rwanda na washirika wengine tunatayarisha vifaa mahitajio kwa ajili ya kuwahudumia”, limeandika shirika la HCR-Rwanda kwenye ukurasa wa Twitter.

Kwanza kabisa, HCR inazidi kuwa kituo kipya kiliandaliwa kwa ajili ya kupokea wakimbizi hao kutoka Kongo sehemu kubwa wakiwa watumiaji wa lugha ya Kinyarwanda kutoka mikoa wa Kivu ya kusini na kaskazini.

” Kituo kipya cha muda kiliundwa eneo la Nkamira karibu na mpaka na RDC kwa ajili ya kuwapokea waomba hifadhi hao na kuwahudumia ” linasema shirika hilo.

Kama linavyohakikisha HCR, kituo hicho kilitayarishwa ili kujiweka tayari kupokea wimbi la wakimbizi wanaoweza kuingia wiki zijazo kufuatia mazingira ya kuogopa uwezekano wa mapigano kurudi kuripotiwa mashariki mwa Kongo kati ya jeshi ya taifa na kundi la waasi la M23.

Baadhi ya wakimbizi wanaongia hupewa hifadhi katika kambi ya muda ya Kijote eneo la Nyabihu na wengine walipelekwa katika kambi la Mahama mashariki mwa Rwanda ambapo wanaishi pamoja na raia kutoka Burundi.

Hivi karibuni, wakimbizi kutoka Kongo walijawa na hofu ikidaiwa kuwa wanaweza kurudishwa kwao kufuatia matamshi ya rais wa Rwanda Paul Kagame akimujibu mwenzake wa Kongo Félix Tshisekedi. Maelezo yalitolewa mapema na ofisi ya rais wa Rwanda ili kujaribu kutuliza mioyo yao.

” Kauli ya rais wa jamuhuri ilichukuliwa visivyo. Tutaendelea kuwapokea watu wanaotoroka wakihofia usalama wao, ukatili na ghasia. Lakini tunaomba jamii ya kimataifa kuchukuwa jukumu katika kutafuta suluhu la kudumu kwa kundi hilo la wakimbizi waliosahawulika wa DRC”, alieleza naibu msemaji wa serikali ya Rwanda Alain Mukurarinda.

Alisisitiza kuwa jamii ya kimataifa na serikali ya Kongo wanatakiwa kuacha kukimbia majukumu yao na kuanza kukabiliana na sababu za uhakika za mzozo huo wa wakimbizi.

Raia wa Kongo wanaokimbia ni wenye asili ya mkoa wa Kivu kaskazini. Jamii ya watutsi wa Kongo wamekuwa waathiriwa wa kauli za chuki kwa jumla, ubaguzi na mateso vinavyosababishwa na itikadi za jenoside ambayo ilisambazwa na makundi ya waliotekeleza mauwaji nchini Rwanda, kundi la FDLR na kuzingatiwa na taasisi za uongozi na usalama wa Kongo.

Kundi la kwanza la wakimbizi kutoka Kongo wanaotoroka mgogoro wa sasa waliwasili nchini Rwanda mwezi novemba 2022 wakati kundi la M23 liliposogelea mji wa Goma makao makuu ya mkoa wa Kivu kaskazini, karibu na kanda ya Rubavu, ndani ya mkoa wa magharibi mwa Rwanda.

Previous Rwanda-DRC : the Rwandan army fired on a Congolese fighter plane
Next Rwanda-DRC : jeshi la Rwanda limeshambulia ndege ya kivita ya Kongo