Burundi : watumiaji wa mtandao wa Ecocash wajawa na hofu

Burundi : watumiaji wa mtandao wa Ecocash wajawa na hofu

Mamlaka ya kukusanya mapato ya serikali (OBR) ilichukuwa udhibiti wa akaunti za kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Econet Wireless Burundi. Watumiaji wa mfumo wake kutuma na kupokea pesa maarufu Ecocash hawana tena uwezo wa kupokea pesa. Mawakala na wakuu wao pamoja na watu binafsi hawajuwi la kufanya. HABARI SOS Médias Burundi

Katika benki zote na taasisi za fedha zinazoshirikiana na mfumo wa Ecocash, hakuna uwezekano tena wa kupokea pesa tangu alhamisi hii tarehe 26 januari 2023 majira ya alasiri.

” Wakati nilipoelekea kwenye benki na Ecocash, wameniambia kuwa hamna pesa. Nimerudi mikono mitupu. Ninajihisi vibaya ninapofikiria pesa ambayo mawakala watapoteza mbali na hali yangu binafsi. Kuna wale watakaopoteza ma milioni ya pesa wakati si pesa yao binafsi “, analalamika wakala mmoja anayefanyia biashara kati kati mwa jiji la Bujumbura, jiji kuu la kibiashara.

Katika maeneo yote, sura za mawakala zinatisha. Baadhi husalimiana kati yao huku huzuni ikionekana kwenye sura zaao. Msichana mmoja alievalia sare ya Ecocash alijieleza, machozi yakitiririka :” Ninaweza kupoteza zaidi ya laki tano wakati ambapo pesa hiyo ninayotumia si ya kwangu. Nitaenda wapi Mungu wangu!”

Wakala mwingine ana matumaini. Kwa mjibu wake, ” serikali ni mzazi wetu. Haiwezi kuiba pesa ya watoto wake. Tuzidi kuwa na matumaini. Jibu litapatikana kesho pengine”.

Mamlaka ya kukusanya mapato ya serikali iliamuru akaunti zote za mtandao wa Econet kutokana na ” deni la bilioni 88 sarafu za Burundi pamoja bilioni 44 dola za kimarekani”. Barua ilioandikiwa taasisi zote za fedha tarehe 24 januari 2023, ilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii alhamisi asubuhi, kabla ya mfumo kuparanganyika. Lakini kampuni hiyo yenye wateja wengi katika nchi hiyo ya afrika mashariki ilituliza kwamba ” mnaweza kuendelea huduma ya Ecocash”.

Hivi karibuni, rais Neva alitahadharisha kuwa ” sintakuwa na huruma kwa makampuni hayo simu za mkononi, hakuna hata msamaha unaolingana na punche moja”. Kulingana na rais wa Burundi, makampuni ya simu za mkononi hutajirika chini ya mgogo wa walipa kodi bila kuchangia chochote kwenye hazina ya serikali wakati ambapo tayari walipata faida zaidi ya mara milioni tano”.

“Daima munadai taratibu za serikali kurithi nyingine. Nani aliwadanganya kuwa serikali inatuhumika katika makosa ?” alifahamisha hayo mwezi disemba iliyopita katika mkoa wa Kayanza kaskazini mwa Burundi. Hayo ni kwa kuzingatia mikataba ya makampuni ya simu za mkononi pamoja na ile ya makampuni ya kuchimba madini.

Bwana Ndayishimiye anasema ni ” mikataba mibovu na ya kimagendo ambayo hawezi kukubali kama rais wa nchi na kuhakikisha kuwa ” nitaisoma mikataba hiyo, na mimi binafsi nitakwenda kuijadili sababu ninapotuma fundi, atapewa rushwa. Mimi mwenyewe nitakuwa wakili mtetezi.

Kampuni hiyo yenye wawakilishi wengi nchini humo haijasema chochote kuhusu hali hiyo. Si mara ya kwanza serikali kutishia kufunga kampuni hiyo iwapo haitalipa madini yake”. Lakini hii ni mara ya kwanza kwa akaunti zake kuchukuliwa.

Previous Beni: at least 18 injured in a recent homemade bomb blast
Next Rwanda-DRC : Kigali inadai kuwa aduwi wake peke katika ukanda huu ni Kinshasa