Rwanda-DRC : Kigali inadai kuwa aduwi wake peke katika ukanda huu ni Kinshasa

Rwanda-DRC : Kigali inadai kuwa aduwi wake peke katika ukanda huu ni Kinshasa

Waziri wa Rwanda wa diplomasia alikuwa bungeni alhamisi kwa ajili ya ” kueleza” wawakilishi hao wa wananchi kuhusu hali ya sasa ya ushirikiano wa Rwanda. Daktari Vincent Biruta alihakikisha kuwa katika ukanda huu , Rwanda ina aduwi mmoja peke ambaye ni DRC. HABARI SOS Médias Burundi

Wajumbe wa mabara za mawili ya wawakilishi ya Rwanda walikuwa tayari kumusikiliza waziri huyo mjumbe wa serikali. Daktari Vincent Biruta aliambatana na naibu msemaji wa serikali ambaye aliwahi kuwa balozi wa Rwanda nchini Kongo aliyefukuzwa na viongozi wa Kongo mwishoni mwa mwezi oktoba 2022.

Bwana Biruta hakupita katika njia za mbali .

” Tulikubaliana na Burundi kuhusu njia za kurejesha uhusiano wetu na mambo yanakwenda vizuri baada ya mikutano mingi. Kaskazini kwenye mpaka na Uganda, uhusiano ni mzuri pamoja pia Tanzania mashariki. Lakini magharibi, hakuna kinachoendelea”, alisema.

Na kuzidi kusema : kaskazini (Uganda) na kusini (Burundi) mipaka wa kipindi fulani ilikuwa imefungwa lakini kwa sasa imefunguliwa na wananchi wanaopita pasina wasi wasi”.

Na kufahamisha kuwa ” kwanza uhusiano ni mzuri na nchi zote za afrika mashariki ispokuwa tu aduwi mmoja ambaye hivi karibuni aliruhusiwa kujiunga na EAC”.

Waziri huyo wa ushirikiano wa kimataifa alisisitiza kuwa ” aduwi huyo” anaweza kubadili hisia zake na ” kukabiliana na matatizo ya kweli na kurudi kuwa rafiki”.

Mzizi…..

Kwa mjibu wa kiongozi wa maswala ya diplomasia, chanzo cha mzozo ni kuibuka kwa mapigano kati ya waasi wa M23 na jeshi la Kongo.

” Kwa hoja tu kuwa baadhi ya wajumbe wa kundi hilo huzungumza Kinyarwanda, na kwamba sababu za kupigana kwao ni kulinda watumiaji wa lugha ya Kinyarwanda, kuomba haki yao na wakimbizi pamoja na wakimbizi kurudi, (…),DRC inatutuhumu kuwaunga mkono, madai ambayo si ya ukweli “, alisisitiza.

Na kuendelea :” kwa hiyo, Rwanda, nchi zingine kama DRC zinaona kuwa hoja hizo ni za msingi. Lakini kwa hakika hatupigani kwa upande wao. Kamwe!”

Suluhisho

” Kuiacha nchi ya Rwanda na kutuchukuwa kama washirika katika kutafuta suluhu la mzozo huo, kutekeleza makubaliano ya Kinshasa yaliyosainiwa, ni mambo ya kawaida”, alisikiliza akisema bwana Biruta.

Kigali inaendelea mbali na kusema kuwa ” DRC inataka kuifanya Rwanda kama ngao kwa ajili ya kuacha kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa, kuonyesha jamii ya kimataifa kuwa kuwa tunawavuruga lakini sio ukweli” alibaini waziri wa diplomasia kabla ya kusisitiza kuwa ” ni nchi hiyo itakayoathirika sana”.

” Harafu DRC unafika ushirikiano wake na kundi la waliofanya mauwaji nchini Rwanda la FDLR ambalo linaonekana bila kufanya uchunguzi wa kina sababu jeshi hilo linawapa silaha na sare “, alituhumu.

Kigali ” tayari”

Naibu msemaji wa serikali upande wake, alitoa ” maelezo ” kuhusiana na matukio ya hivi karibuni hususan lile la ndege ya kivita ya Kongo kushambuliwa na jeshi la Rwanda wiki hii.

” Tunaridhishwa na hilo.Ni kulinda mipaka ya nchi ya Rwanda. Jeshi letu linafahamu vizuri hilo, liko tayari kuonyesha hilo kila wakati. Tulikuwa tumejizuia […] mipaka ya Rwanda ya ardhini na angani imelindwa vya kutosha”, alisisitiza Alain Mukurarinda.

Rwanda inafahamisha utayari wake kwa aina yoyote ya mazungumzo na kuahidi kuunga mkono juhudi za kikanda za kumaliza mzozo wa Kongo.

Uhusiano kati ya mataifa hayo mawili ya maziwa makuu ya Afrika unazidi kuzorota tangu kuibuka tena kwa kundi la machi 23, kundi la M23.

Kundi hilo la waasi wa kabila la watutsi lilichukuwa tena silaha mwishoni mwa 2021 likituhumu viongozi wa Kongo kutotekeleza ahadi za kuhusu kuwarejesha katika maisha ya kawaida wapiganaji wake ambao ni watutsi wa Kongo.

Viongozi wa Kongo wanakubaliana kuwa kundi hilo linapata usaidizi kutoka Rwanda, madai ambayo serikali ya Rwanda inazidi kukanusha na kutupilia mbali. Rwanda upande wake iliendelea kutuhumu FARDC ( jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo) kushirikiana na wauwaji wa kundi la FDLR” kwa lengo la kuvuruga ardhi yake”.

Lakini rais wa Kongo Félix Tshisekedi kwa mara nyingi akimtuhumu mwenzake wa Rwanda Paul Kagame ” kuunga mkono waasi hao na kudai kuwa kundi la FDLR sio tishio tena kwa Rwanda na kulita kama kundi la wezi”.

Previous Burundi : watumiaji wa mtandao wa Ecocash wajawa na hofu
Next Nyarugusu (Tanzania): mkimbizi mwenye asili ya Burundi alipatikana akiwa maiti