Nyarugusu (Tanzania): mkimbizi mwenye asili ya Burundi alipatikana akiwa maiti
Mkimbizi kutoka Burundi mwenye umri wa miaka takriban miaka 40 aliuwawa na watu wasiojulikana karibu ya kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu nchini Tanzania. Polisi inasema ni tukio la wizi lililokwenda vibaya. Watu wengi walisimamishwa kwa ajili ya uchunguzi. HABARI SOS Médias Burundi
Antoine Nsengiyumva mkaazi wa village 7 zone 11 katika kambi ya Nyarugusu nchini Tanzania. Muili wake uligunduliwa katika shamba la nyanya karibu na kambi hiyo.
Huenda akawa mjumbe wa genge la majambazi kulingana na polisi.
” Huenda alikuwa katika genge la majambazi watatu. Walienda kuiba katika shamba la nyanya nje ya kambi. Wamiliki wa shamba hilo pamoja na walinzi huenda waliwakamata wezi hao. Washirika wake walifanikiwa kukimbia na yeye akakamatwa na kupigwa hadi kufa. Alipata pia majeraha kwa kupigwa mapanga”, polisi ilifahamisha hayo na kuwaomba kuacha wizi na wakimbizi kuacha kujichukulia sheria mikononi katika kambi ya Nyarugusu na maeneo ya karibu.
” Pembeni ya maiti hiyo, kuliogotwa kitunga kinachojaa nyanya na vituguu ambavyo vilivunwa ndani ya shamba hilo na hivyo kuonekana kuwa taarifa za kuwa ni tukio la wizi lililokwenda vibaya zinaweza kuwa za ukweli”, polisi inazidi kufahamisha.
Polisi iliwaitisha wamiliki wote na walinzi wa mashamba ya karibu na eneo hilo ambako maiti hiyo ilipatikana. Uchunguzi tayari umeanzishwa.
Muhanga aliacha mjane na watoto watatu katika kambi ya Nyarugusu ambayo inawapa hifadhi zaidi ya wakimbizi elfu 50 kutoka Burundi.
You might also like
Burundi : 20 scholarships for hundreds of young refugees, DAFI rekindles hope
SOS Médias Burundi Muyinga, August 11, 2026 — After a two-year hiatus due to funding difficulties, the DAFI (Albert Einstein German Academic Refugee Initiative) scholarship program is reopening its call
DRC : in Lusenda, Burundian refugees say they are abandoned under tarpaulins after years of waiting
SOS Médias Burundi Uvira, July 16, 2026 – After several years living in severely dilapidated shelters, hundreds of Burundian families living in the Lusenda camp, in the Fizi territory of
Giharo : the district police commissioner killed with machetes
Police Major Japhet Mukeshimana was killed on the evening of Tuesday, January 2, 2024. The tragedy took place in Nkanka village in Giharo district in Rutana province in southeast Burundi.
