Bujumbura : chama cha CNL chazuiliwa kuadhimisha kumbukumbu ya miaka minne

Bujumbura : chama cha CNL chazuiliwa kuadhimisha kumbukumbu ya miaka minne

Waziri wa mambo ya ndani na usalama aliamuru kupiga marufuku sherehe za maadhimisho ya miaka minne ya uhai wa chama cha CNL na zile za kutakiana rheli za mwaka mpya kwa wafuasi wa chama hicho zilizopangwa kufanyika tarehe 19 februari. Mzozo unaweza kutokea kwenye eneo la sherehe na katika njia ya washiriki. Kiongozi wa chama cha CNL Agathon Rwasa anafahamisha kuwa maswala yanayoweza kusababisha mzozo yalipata majibu katika mkutano uliofanyika tarehe 17 na 18 mjini Bujumbura. HABARI SOS Médias Burundi

Katika barua iliyotumwa kwa mwenyekiti wa chama cha CNL, waziri wa mambo ya ndani na usalama anafahamisha kuwa tarehe 15 februari alifanya mazungumzo na mpinzani wa kihistoria Agathon Rwasa. Mkutano huo ulihusu ” kundi la wajumbe wa ofisi kuu ya kisiasa wanaotuhumiwa mpango wa mapinduzi dhidi ya taasisi za chama”.

Waziri Martin Niteretse alikumbusha kuwa walikubaliana na mkuu wa chama cha CNL kuwa atakutana na wasaliti na kuwaambia matokeo ya mkutano wake na waziri kwa ajili ya ” kuwahakikishia kuhusu swala la usalama wa sherehe hizo”.

” Kwa bahati mbaya, hadi sasa hatujawasiliana, hali inayopelekea kufikiria kuwa hamkuweza kupata suluhu ya mzozo. Kwa sababu hiyo katika lengo la kukinga malumbano kwenye eneo la sherehe na njiani kwa washiriki, ninawataarifu kuwa sherehe (…)imesimamishwa ” alieleza waziri.

Anafahamisha kuwa magavana wa mikoa na meya wa jiji la Bujumbura ( mji mkuu wa kiuchumi) pamoja na inspekta mkuu wa polisi wanatakiwa kuheshimu muongozo huo.

Jumamosi hii, ofisi kuu ya chama hicho kikuu cha upinzani imetoa tangazo ambamo inafamisha kuwa mgogoro wao ulipata majibu kwa sehemu kubwa huku likisubiriwa jibu la kudumu. Tangazo linataja kuwa ” ni hali ya kutoelewana “.

Katika ujumbe wa sauti, Agathon Rwasa anafahamisha kuwa maswala yanayoweza kusababisha mzozo yalipatiwa jibu katika mkutano wa siku mbili.

” Tulifanya mkutano ijumaa saa tisa na hatukuweza kumaliza maswala yote yaliyokuwa kwenye agenda. Tulikutana tena jumamosi akiwepo muakilishi wa waziri. Tulifikia makubaliano na tukatoa tangazo ambamo tulimuomba kuturuhusu kuandaa sherehe hizo sababu tulifanya yale tuliokuwa tumemuahidi na hali iliendelea vizuri”, alifafanua bwana Rwasa.

Na kuzidi kusema ” pamoja na hayo , wote waliona barua ya waziri kwa wakuu wa tarafa na magavana wa mikoa. Pointi ya tisa ya barua hiyo, inasema kuwa wanatakiwa kuruhusu vyama vya kisiasa kuongoza harakati zao pasina kuzuiliwa. Tunamuomba kutuelewa sababu baadhi ya wajumbe tayari wamewasili mjini Bujumbura. Hapatakuwa tatizo.

Ofisi ya waziri Niteretse inayohusika na mawasiliano haikuwa karibu ili kuweza kujibu madai hayo ya mpinzani wa kihistoria Agathon Rwasa.

Chanzo katika wizara ya usalama kimeambia SOS Médias Burundi kuwa ” sherehe hizo hazitafanyika”.

” Tunawajuwa, ni wajanja sana. Wanawaza kutangaza kuwa sherehe zitafanyika kwenye ofisi ya chama eneo la Mutanga wakati ambapo zimepangwa kufanyika eneo la Ngagara. Ni kwa sababu hiyo barabara zote zinazoelekea kwenye ofisi kuu za chama hicho zitakuwa zimefungwa siku ya jumapili. Hakuna ofisi ya chama ambayo itaruhusiwa kufunguliwa siku ya jumapili mjini Bujumbura, chanzo hicho kinazidi kusema.

Lakini Rwasa anasisitiza : ” itakuwa sheria kwetu sisi wote iwapo wataturuhusu kuandaa sherehe hizo sababu upande wetu changamoto zote ziliondolewa”.

Previous DRC-EAC: en route to the establishment of a monitoring and verification mechanism in eastern DRC
Next RDC-EAC: mchakato wa kuhakiki na kufuatia hali mashariki mwa DRC unaelekea kuanzishwa