RDC-EAC: mchakato wa kuhakiki na kufuatia hali mashariki mwa DRC unaelekea kuanzishwa

RDC-EAC: mchakato wa kuhakiki na kufuatia hali mashariki mwa DRC unaelekea kuanzishwa

Jumuiya ya Afrika mashariki inapanga kutuma wajumbe wa mchakato wa kuhakiki na kufuatia hali mashariki mwa DRC ambao ni muhimu sana ili kumaliza mzozo. Hayo ni kulingana na tangazo lililowekwa kwenye anuani ya EAC ijumaa hii. Katika mkutano wa wakuu wa nchi, wakuu wa majeshi wa nchi wanachama wa EAC, waliamuru kuteuwa tume kwa ajili ya kufuatia utekelezwaji wa maagizo ya mkutano wa marais uliofanyika katika jiji la kibiashara la Burundi Bujumbura. HABARI SOS Médias Burundi

Wakuu wa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika walikutana mjini Bujumbura katika mkutano wa dharura ulioitishwa na rais Ndayishimiye ambaye pia ni mwenyekiti wa EAC.

Mkutano huo kuhusu hali ya usalama mashariki mwa Kongo uliamuru mapigano yasimame mara moja na kundi la waasi liondoke katika maeneo linaloshikilia na pia mazungumzo yafanyika kati ya pande hasimu. Wakuu wa majeshi ya nchi za jumuiya hiyo waliamuru kuteuwa timu ya kufuatilia utekelezwaji.

” Ninapongeza uamuzi wa wakuu wa majeshi ya kutuma wajumbe wa mchakato wa kufuatilia na kuhakiki wa jumuiya ya afrika mashariki (EAC-MVM) ili kuchunga na kukagua utekelezwaji wa hatua ya kusitisha mapigano na kuondoka kwa vikosi vya waasi”, linafahamisha tangazo lililowekwa kwenye anuani na katibu mkuu wa jumuiya hiyo ijumaa hii.

Kwa mjibu wa tangazo hilo, ofisi ya katibu inajihusisha zaidi na mzozo huo pamoja na nchi zote wajumbe na wadau wengine ili kuongeza kasi ya kutuma wajumbe wa mchakato huo” ambao una jukumu kubwa katika kumaliza makabiliano”.

” Mchango wa ofisi ya katibu mkuu wa EAC kuhusu kurejesha amani na utulivu mashariki mwa DRC ni muhimu”, tangazo hilo linasema.

Jumuiya ya Afrika mashariki ambayo Kongo imekuwa mwanachama tangu mwaka jana tayari jumuiya ya Afrika mashariki ilituma wanajeshi katika baadhi ya maeneo ya mzozo wa silaha katika kanda ya mashariki mwa DRC zikiwemo wilaya nyingi za mkoa wa Kivu kaskazini.

Lakini kikosi hicho kinakosolewa na sehemu ya wadau wa Kongo wanaotuhumu kikosi hicho ” kutowajibika, na kuegemea upande ” kwa hoja kuwa hakijashambulia kundi la M23, kundi la silaha lililochukuwa udhibiti wa maeneo mengi ya mkoa tangu juni 2022. Mandamano mengi yalifanyika katika mikoa ya Kivu-Kusini na Kivu-kaskazini kwa lengo la kulaani kikosi hicho na kuomba kuondoke “.

Wakati wa mkutano wa kilele wa Bujumbura, rais Tshisekedi alionekana ndani ya Vidéo akipandisha sauti dhidi ya kikosi cha EAC na kamanda wake pia.

” Hamkuja ili kupendelea kundi la M23 na ni masikitiko kuona wananchi wakiwashambulia. Mulikuja kutusaidia , hamkuwasili ili mupate matatizo. Kwa hiyo kuweni makini kwa hilo. Jibu maswali ya wananchi, wasiliana na wananchi”, alisisitiza rais wa Kongo akimuambia jemedari Jeff Nyagah kutoka Kenya akiwa pamoja na mwenzake wa Kenya William Ruto.

Previous Bujumbura : chama cha CNL chazuiliwa kuadhimisha kumbukumbu ya miaka minne
Next Photo of the week : Burundi : Burundian authorities have arrested the fifth activist and sent to jail the team suspected of funding terrorism