Mahama (Rwanda) : huduma mbaya za matibabu

Mahama (Rwanda) : huduma mbaya za matibabu

Wakimbizi katika kambi ya Mahama wanalalamika kuwa hupewa huduma mbaya za matibabu kwenye vituo vya afya. Hali za dharura ndizo zinashughulikiwa peke. Hayo ni wakati mratibu mpya katika sekta ya afya alikuwa ameahidi kuleta maendeleo ya sekta hiyo. HABARI SOS Médias Burundi

Kwenye vituo vya afya ndani ya kambi ya Mahama, milolongo mirefu ya wagonjwa wanaosubiri kupata huduma za afya hushuhudiwa. Wanalaani kuwa hupewa huduma mbaya za matibabu.

” Idadi ndogo ya wagonjwa ndio wanaopokelewa huku wanaopewa kipau mbele wakiwa wale waliokuwa katika hali mbaya zaidi. Nilijielekeza kwenye kituo cha afya katika zone ya Mahama ll chini ya uangalizi wa Save the Children. Walikuwepo zaidi ya watu 60 wanaosubiri kupewa huduma tangu siku moja kabla ya siku hiyo. Mtoto wangu asingetapika mbele ya wauguzi, singepokelewa”, alilalamika mkimbizi mmoja kutoka Burundi.

Muhusika aliamuru kuwasiliana na viongozi wa kijamii ili wajihusishe na hali hiyo ambayo anasema ” haikubaliki “. Alituma ujumbe kwenye kundi la WhatsApp ya viongozi wa zone na village (maeneo ya kambi). Ujumbe huo ulifuatiliwa na kuwasilishwa kwa viongozi hao na badaye wakawasiliana na HCR pamoja na shirika la Save the Children.

Wakimbizi waliowasiliana na SOS Médias Burundi wanaomba HCR kuhakikisha kuwa sekta ya afya inawajibika vizuri.

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, sekta ya afya inaratibiwa na shirika la Save the Children lililochukuwa nafasi ya shirika lisilo la kiserikali la Alight ndani ya kambi ya Mahama.

Wakimbizi walikuwa na matumaini kuwa kutakuwa na nafuu maana shirika la Alight halikuwajibika hususan wakati wa janga la Covid-19 kulingana na wakimbizi.

” Tunaomba mabadiliko na tofauti na mratibu wa zamani iweze kuonekana. Wafanyakazi wa Alight walikuwa wakitupatia huduma mbaya wakati wakijihusisha na vijiji 10 vya zone I. Kwa vile shirika la Save the children ndilo litajihusika na eneo lote, linatakiwa kuonyesha nguvu zaidi”. walibaini wakimbizi kutoka Burundi.

HCR ilisema kuwa mabadiliko yalifanyika kwa lengo la kuboresha huduma zinazotolewa katika sekta ya afya” na kudai kuwa na matumaini kwamba kasoro zitasahihishwa”.

Kwa sasa, wakimbizi kutoka Burundi na Kongo wanatoa wito kwa shirika hilo la umoja wa mataifa kufuatia kwa karibu sekta hiyo muhimu.

Sababu ya kutoa huduma mbaya ni kwa vile shirika la Save the children halina wafanyakazi wa kutosha na kutojiandaa kuhudumia kambi yote ambapo idadi ya wakimbizi iliongezeka haraka kutokana na ujio wa wakimbizi wapya kutoka Kongo. Shirika hilo liliahidi kuajiri wafanyakazi wapya mnamo siku zijazo kwa lengo la kuboresha huduma zake ndani ya vituo vya afya katika kambi ya Mahama ambavyo vitawapokea na kuwahudumia jamii ya wanyarwanda wanaoishi karibu ya kambi hiyo.

Kambi ya Mahama inayopatikana mashariki mwa Rwanda inawapa hifadhi wakimbizi zaidi ya elfu 50 idadi kubwa ikiwa ni wakimbizi kutoka Burundi.

Previous Kirundo : kiongozi wa Imbonerakure azuiliwa jela
Next Mahama (Rwanda) : poor quality of health services