Kirundo : kiongozi wa Imbonerakure azuiliwa jela

Kirundo : kiongozi wa Imbonerakure azuiliwa jela

Kiongozi wa Imbonerakure (mjumbe wa tawi la vijana la chama cha CNDD-FDD) mkaazi sa kata ya Nyange-Bushaza kwenye makao makuu ya Kirundo (Kaskazini mwa Burundi) amemaliza wiki moja akiwa katika gereza la polisi ya Kirundo. Sababu za kukamatwa kwake : ni kuendesha vipigo dhidi ya watu watatu akiwemo kiongozi wa kitongoji kinachopatikana katika kijiji hicho pamoja na mwanamke aliyekuwa akibeba mtoto mgongoni. Taasisi ya sheria imepata wahanga wa ukatili wake 21 bila kutaja visa vya mauwaji ambapo jina lake linatajwa. HABARI SOS Médias Burundi

Mkuu wa Imbonerakure katika kata ya Nyange-Bushaza anajulikana kwa jina maarufu la Madora.

Kwa mjibu wa Imbonerakure, alimpiga naibu kiongozi wa kijiji Thadée kwa kosa la kukataa kufunga mgahawa wake wakati ambapo ilikuwa saa mbili na nusu usiku tarehe 14 februari iliyopita.

” Haunitishi. Ninaweza kukupiga kofi na kukubali yatakayotokea “alijigamba Madora.

Mara baada ya kutamka hayo, alitenda. Madora hakuchelewa kumpiga ngumi mbili kichwani na mtu huyo alipoteza fahamu mbele ya mke wake, watoto na wateja wake”, shahidi aliyeshuhudia kisa hicho alieleza.

Baada ya kuona yaliyotokea kwa mteule huyo katika kijiji hicho, mkuu huyo wa Imbonerakure alikimbia.

Vyanzo vyetu vinaarifu kuwa wakati akikimbia, alimusukuma na kumpiga mama mmoja mkaazi wa kata hiyo aliyekuwa na mtoto mgongoni. Mama huyo alianguka chini na mtoto akanusurika kifo.

” Mtoto alipoteza fahamu kwa kipindi cha dakika 45. Tulitoa taarifa kwa polisi na wakawasili haraka lakini walikuwa tayari amekimbia”, alihakikisha shahidi eneo hilo.

Muhalifu huyo alikamatwa siku moja badaye kulingana na vyanzo vya ndani.

Muathiriwa alipelekwa usiku huo huo kwenye hospitali ya mkoa. Gharama za matibabu zinakadiriwa kuwa 87 elfu. Zililipwa na Madora.

Vyanzo vyetu vinafahamisha kuwa afisa wa polisi ya kufuatilia wahalifu aliomba Madora kulipa kitita cha laki mbili na elfu kumi za fidia ili aweze kuachiliwa huru.

Jaji mkuu katika korti kuu ya rufaa ya Ngozi (kaskazini) alipinga kuachiliwa kwake sababu anakabiliwa na kesi zingine.

Jaji huyo alibaini kuwa watu watatu wanaongezeka kwenye orodha ya watu 21 walioathiriwa na ukatili wake.

Madora anatajwa katika visa vya mauwaji yakiwemo mauwaji ya aliyewahi kuwa mkuu wa tarafa ya Kirundo Serges Barutwanayo aliyeuwawa kikatili mwaka wa 2014.

Wakaazi wa mkoa wa Kirundo wanaomba adhabu kali zichukuliwe dhidi ya Madora aliyekuwa katili ndani ya kata hiyo kwa mjibu wao.

Previous Masisi: wakaazi wanaomba amani kupatikana kabla ya kujiandikisha kwenye uchaguzi
Next Mahama (Rwanda) : huduma mbaya za matibabu