Masisi: wakaazi wanaomba amani kupatikana kabla ya kujiandikisha kwenye uchaguzi
Wananchi wakaazi wa wilaya ya Masisi katika mkoa wa Kivu-kaskazini wanatoa wito kwa viongozi kumaliza tatizo la usalama mdogo kabla ya kuanza kwa zoezi la kuorodhesha wapiga kura eneo hilo la mkoa wa Kivu-kaskazini. HABARI SOS Médias Burundi
Baadhi ya wakaazi wa kitongoji cha Mupfunyi-Karuba walihakikisha kuwa watajiandikisha wakati usalama utakuwa umerejea katika eneo hilo.
“Tutaanza kujiorodhesha wakati usalama utakuwa umeimarika ndani ya wilaya ya Masisi. Tuko katika hali mbaya ya usalama”, alibaini Gervais Bahati mkulima wa eneo la Karuba.
Kwa mjibu wake, haiwezekani kujiandikisha wakati ambapo wananchi wa Kongo wengi eneo hilo waliyatoroka makaazi yao.
” Jambo la kwanza ni kuona wananchi wenzetu wanaoishi katika kambi za wakimbizi wa ndani wakirejea katika maeneo yao ya asili. Hatuwezi kuanza kujiorodhesha wakati ambapo ndugu zetu wakiteseka ndani ya kambi wilayani Nyiragongo na maeneo mengine” alilalamika baba wa familla.
Jean Bosco Sebishishimbo Rubuha mbunge aliyechaguliwa eneo la Masisi anafahamisha kuwa serikali inatakiwa kumaliza tatizo la usalama mdogo ndani ya mkoa harafu badaye litafuata zoezi la kuandikisha wapiga kura”.
Idadi kubwa ya wananchi walitoroka mapigana na hawana njia ya kuwasili kwenye vituo vya kujiandikisha “, alifafanua mwakilishi huyo wa wananchi.
” Hatuelewi namna serikali yetu inaweza kuanza mchakato wa uchaguzi bila kujali maisha ya kila siku ya wananchi wa Kongo kwa jumla na hususan maisha wakaazi wa mkoa wa kivu kaskazini. Kwa mtanzamo wetu, usalama ni jambo la msingi, uandikishaji ni badaye”, alisisitiza.
Uandikishaji wa wapiga kura katika eneo la mashariki mwa Kongo ulianza alhamisi iliyopita. Mbali na katika miji kadhaa ambako wajumbe wa jamii ya wanaotumia lugha ya Kinyarwanda na kirundi wanaoishi nchini DRC pamoja pia na watutsi wa Kongo na wajumbe wa jamii ya Banyamulenge walijikuta wakinyimwa haki yao ya kujiandikisha mchakato unaendelea vizuri. Viongozi tawala walikataza wanzilishi wa vuguvugu linalotoa mwito kwa raia wengine wa Kongo na wajumbe wa CENI ” kuwatenga watu wa jamii hizo”.