Uvira : mwanajeshi mmoja na wananchi wawili wauwawa

Uvira : mwanajeshi mmoja na wananchi wawili wauwawa

Raia wawili wa kawaida, waliuwawa na watu wanaobebelea silaha. Na mwanajeshi mmoja wa Kongo pia aliuwawa. Waliouwawa walikuwa miongoni mwa kundi la vijana walinzi wa amani wanaofanya doria usiku. Mwanajeshi huyo upande wake, alipigwa na wananchi. HABARI SOS Médias Burundi

Hali hiyo ilianza jumamosi jioni katika kata ya Kasenga. Ni katika mji wa Uvira katika mkoa wa Kivu ya kusini mashariki mwa DRC.

Wezi wanaotumia silaha walijaribu kuiba katika maduka, vijana walinzi wakawafuatilia. Kijana mmoja aliuwawa wa watu hao wanaobebelea silaha. Katika kuwafuatilia, wezi hao , vijana hao walinzi wa amani, walipofika mbali, walikutana na wanajeshi wa Kongo, vijana hao wakishirikiana na wakaazi wengine wakawakabili wanajeshi hao. Wakajaribu kumpiga mawe mwanajeshi anayetuhumiwa kujumuika na genge hilo la wezi. Alipelekwa kwenye hospitali ya Uvira akiwa katika hali mbaya.

Jumapili asubuhi, hali hiyo iliibuka tena. Wakati vijana hao wakipeleka muili wa ndugu yao wakakutana na askali jeshi na kumushambulia na kutaka kumpiga mawe. Alifuatua risasi dhidi yao na kuwauwa wawili kati yao.

Wakaazi walimufuatilia mwanajeshi huyo na kumuuwa kwa kumpiga mawe. Kupitia tangazo, jeshi la Kongo linathibitisha kifo cha mwanajeshi huyo na wananchi wawili na kuzidi kuwa watu wengi watatu akiwemo mwanajeshi mmoja walijeruhiwa.

” Mwanajeshi huyo alikuwa katika hali mahtuti ” , jeshi la Kongo linafahamisha na kukumbusha kuwa usalama wa wananchi na mali zao ni jukumu la taasisi za ulinzi na usalama “.

Wakaazi wa mkoa wa Kivu kusini waliozungumza na SOS Médias Burundi wanawaomba viongozi wa Kongo” kusimamisha shughuli za vijana walinzi wa kawaida ambao wana utawala usiokuwa na mipaka”.

Kamanda wa sekta ya operesheni ya Sokola 2 anataja kisa hicho kilichosababisha kifo cha mwanajeshi kuwa ni kitendo dhidi ya uzalendo.

Previous DRC-Rwanda: cross-border trade slowly takes up between Goma and Gisenyi after the death of a Congolese soldier
Next Dzaleka (Malawi) : four Burundian refugees detained on suspicion of organizing a demonstration