Cibitoke: miili tisa ya waasi wa Rwanda ilipatikana katika msitu wa kibira
Alasiri siku ya ijumaa, walinzi wa msitu waliona miili tisa ikianza kuharibika kwenye mlima wa Gafumbegeti. Ni katika kijiji cha Butahana tarafani Mabayi mkoa wa Cibitoke (kaskazini-magharibi mwa Burundi). Kijiji hicho kinapataka na msitu wa Kibira. Wakaazi wa kijiji hicho wanasema kuwa maiti za waasi wa Rwanda zimekuwa zikigundulika. HABARI SOS Médias Burundi
Mapigano ya mwisho kati ya jeshi la Burundi na waasi wanaopambana dhidi ya Kigali yalipelekea angalau waasi tisa kuuwawa kwa mjibu wa vyanzo vyetu.
” Niliona miili inayoanza kuharibika ya watu wanaovalia sare za jeshi la Kongo siku ya ijumaa alasiri tarehe 2 disemba kwenye mpaka wa msitu wa Kibira [….]” alitoa ushuhuda huo mlinzi wa msitu mmoja ambaye alikuwa wa kwanza kuona miili hiyo na kuwaambia wenzake.
Chanzo cha kijeshi upande wake, kinahakikisha kuwa mapigano makali kati ya jeshi la Burundi na waasi wa Rwanda wakiwa na makao yao nchini DRC yalipelekea jeshi la FDNB kukamata silaha nzito na zile ndogo ndogo nyingi”
Ngome zao nyingi zilikamatwa pia. Zilikuwa zinakaliwa na waasi tangu mwaka wa 2015″.
Kiongozi tawala mmoja anathibitisha hali hiyo.
” Waakazi wengi walikimbia majumba yao. Wanapewa hifadhi kwenye makao makuu ya tarafa ya Mabayi”, anasema.
Afisa mkuu anayehusika na operesheni za kijeshi tarafani Mabayi na Bukinanyana anahakikisha taarifa hizo na kudai kuwa matokeo ya operesheni hiyo ni ya kuridhisha. Anafahamisha pia kuwa ” wanajeshi wetu kwa sasa wanaendesha operesheni za kumalizia mahala popote ambako bado waasi wanaendelea kujihami huku wengi wakiwa walikimbia”. Anawaomba wananchi kushirikiana na jeshi katika kuimarisha usalama kwa kufichuwa kila kitu kinacholeta wasi wasi.
Akiulizwa kuhusu hali hiyo, mkuu wa tarafa ya Mabayi, Nicodème Ndahabonyimana anathibitisha habari hizo na kuzidi kuwa ” milio ya sihala nzito imekuwa ikisikika mara kwa mara mnamo siku zilizopita katika msitu wa hifadhi wa Kibira”.