Bubanza: vijana Imbonerakure wapiga mwanaume mmoja hadi kufariki akiwa hospitali

Bubanza: vijana Imbonerakure wapiga mwanaume mmoja hadi kufariki akiwa hospitali

Lionel Nzoyisaba alikuwa akijulikana kama mwizi tarafani Mpanda mkoa wa Bubanza. Alikuwa akiiba simu katika maduka eneo hilo. Usiku wa kuamkia tarehe mosi disemba, Nzoyisaba alisimamishwa na vijana Imbonerakure akitoka kuiba ndani ya duka moja. Walimuchapa. Mwishowe, alifariki dunia akiwa kwenye hospitali ya Mpanda, mkoa wa Bubanza (magharibi mwa Burundi). HABARI SOS Médias Burundi

Kisa cha mwisho cha wizi wake kilikuwa siku ya ijumaa.

” Mwanamke mmoja alifunga duka lake bila kujuwa kuwa Lionel alikuwa ndani. Wakati akijaribu kutoka akiwa na bidhaa alizoiba, jirani alimukamata na kuomba msaada ” alifafanua jirani mwingine mkaazi wa kitongoji cha Nyabikere katika kijiji cha Musenyi.

Baada ya kusimamishwa na vijana wafuasi wa chama tawala, Lionel Nzoyisaba alipelekwa kwenye mto Gifugwe katika kijiji hicho. Vijana hao walimpiga kinyama.

” Walimumwagia maji muilini ili ateseke wakati akichapwa. Mtu huyo walimurudusha akiwa katika hali mbaya. Afisa wa polisi aliyemuhoji, alimutia jela badala ya kumupeleka moja kwa moja hospitali. Usiku huo huo akiwa katika hali mahtuti, alipelekwa kwenye hospitali kuu ya Mpanda na kufa akiwa kwenye hospitali hiyo, vyanzo vyetu vinahakikisha.

Mke wa muhanga huyo anawatuhumu viongozi wa tarafa ya Mpanda, mkuu wa kijiji cha Musenyi ” nia ya kutaka kuzimisha kisa hicho na kuacha kuwafuatilia Imbonerakure wanaotuhumiwa katika mkasa huo”.

” Nimemkosa mume wangu ambaye alikamatwa na Imbonerakure, na kupigwa katika usiku huo. Na badala ya kuwakamata watuhumiwa wa maovu hayo, wanasema kuwa kifo hicho hakina maana kwao”, anakosoa mke huyo wa hayati.

Previous Cibitoke: miili tisa ya waasi wa Rwanda ilipatikana katika msitu wa kibira
Next Burundi: angalau 25% ya wandishi wa habari walipewa kadi