Burundi: angalau 25% ya wandishi wa habari walipewa kadi

Burundi: angalau 25% ya wandishi wa habari walipewa kadi

Baraza la CNC (baraza la uandishi wa habari) siku ya ijumaa ilizindua rasmi shughuli ya kutoa kadi mpya ya uandishi wa habari. Ni idadi ndogo ya wandishi walioweza kupata kadi hiyo. CNC inafahanuwa kuwa sababu kuu ni faili za wahitaji zisizoeneza vigezo au kucheleweshwa. HABARI SOS Médias Burundi

Kwa angalau wandishi elfu moja waliowasilisha maombi ni 240 pekee waliopewa kadi, kulingana na Vestine Nahimana kiongozi wa CNC.

” Kadi zilizotolewa ni chache ukilinganisha na idadi ya walioomba wanaokadiriwa kuwa elfu moja. Idadi kubwa ya wandishi wa habari hawakuweza kupata kadi hiyo sababu hawatimizi vigezo vinavyohitajika ili kupata kadi ya uandishi wa habari. Wengine hawakuwasilisha faili kwa wakati, alifafanua.

Kwa wale waliopata kadi hiyo, aliwaomba kuitumia vizuri.

[….] kadi hiyo inawafungulia milango wandishi wa habari ili kufikia vyanzo vya habari” alisisitiza mama Nahimana.

Moja kati ya masharti ili kupata kadi hiyo mpya wa wandishi wa habari, ni kuwa na mkataba wa kazi na kulipa pesa elfu 15 sarafu za Burundi na na kurudisha kadi ya zamani.
Kadi mpya itakuwa na muda wa miaka mitano.

Tangu mzozo wa 2015 uliosababishwa na muhula mwingine ulioleta utata wa rais Pierre Nkurunziza, viongozi wa Burundi walituhumiwa mara nyingi ” kunyanyasa vyombo vya habari”.

Lakini katika miaka mitatu iliyopita, nchi hiyo ndogo ya afrika ya mashariki ilipanda kwa alama ya rikodi ya kuheshimu uhuru wa habari inayotolewa na shirika la RSF ( ma ripota wasio na mipaka) na kutoka kwenye nafasi ya 160 na kurudi nyuma kwenye nafasi ya 107.

Rikodi hiyo inatathimini mazingira ya uendeshaji kazi ya uandishi wa habari katika nchi na maeneo 180.

Previous Bubanza: vijana Imbonerakure wapiga mwanaume mmoja hadi kufariki akiwa hospitali
Next Nakivale (Uganda): torrential rains cause injuries and material damage