Lusenda-Mulongwe : njaa yapiga hodi katika kambi za wakimbizi kutoka Burundi

Lusenda-Mulongwe : njaa yapiga hodi katika kambi za wakimbizi kutoka Burundi

Wakimbizi wa kambi za Lusenda na Mulongwe katika wilaya ya Fizi mkoa wa Kivu ya kusini mashariki mwa DRC wanasema kuwa wanakabiliana na uhaba wa chakula. PAM (WFP) shirika la mpango wa chakula duniani ambalo huwapatia msaada wa chakula, sasa ni miezi mitatu pasina kuwapa chakula. Wanahofia baa la njaa katika eneo hilo la Kongo ambapo maafisa wa usalama wanawaomba kuacha kutoka nje ya kambi kwa hofu ya kushambuliwa na kuuwawa na makundi ya silaha. HABARI SOS Médias Burundi

Kawaida shirika la PAM huwapa pesa wakimbizi ili waweze kununua wenyewe chakula wanachohitaji. Lakini sasa ni miezi mitatu bila wakimbizi hao kupewa msaada huo.

” Idadi kubwa kati yetu waliuzisha vifaa vya ndani ili kuendelea kuishi “, wakuu wa familia walisema.

Kwa mjibu wa Rémy Habumuremyi, muakilishi wa watu wanaotembea na ulemavu eneo la Lusenda, hali hiyo imewaathiri idadi kubwa na wajumbe wa shirika hilo.

” Hatuwezi kutoka nje ya kambi kwa ajili ya kutafuta kazi kwa raia wa Kongo” , analalamika.

Hali hiyo imepelekea wanafunzi kuacha shule kama alivyofanya kijana Rashidi.

” Nililazimika kuacha shule na kwenda kutafuta kazi kwa wavuvi katika ziwa Tanganyika sababu familia yangu inakabiliwa na umasikini mkubwa. Bila msaada wa chakula, familia haiwezi kuwapa chakula mimi na ma Kaka na dada zangu”, kujana huyo alitoa ushuhuda huo.

Baadhi ya akinamama kama Evelyne Kubwimana hushinda kutwa nzima kwenye fukwe la ziwa Tanganyika. Anaandaa chakula kwa ajili ya wavuvi.

” Hii inanisaidia kupata pesa ndogo kwa ajili ya kununua unga wa kusonga uhalifu na mboga za kutumia kwa watoto wangu”, alifafanua mwanamke huyo mwenye asili ya Burundi.

Katika kambi ya Lusenda, kila mkimbizi hupewa sarafu za Kongo 19500 kwa gharama ya chakula cha kila mwezi. Wakimbizi wanasema pesa hiyo “haitoshi”.

” Bei ya vyakula imepanda kwa kiwango kikubwa”, wakimbizi wanasema.

Hali ni kama hiyo katika kambi ya Mulongwe

Marie Kubwimana ni mkimbizi kutoka kambi ya Mulongwe. Anafahamisha kuwa alijiandikisha kwenye orodha ya wale wanaopendelea kurudi nchini kwa sababu ya ukosefu wa vyakula.

François Nizigiyimana pia alichukuwa msimamo huo. Kutokana na hali hiyo, wakimbizi wengi kutoka Burundi, wanaanza kuomba msaada nje ya kambi hususan kwenye fukwe za ziwa Tanganyika.

SOS Médias Burundi haikukufanikiwa kuwapata viongozi wa PAM ili wafafanuwe sababu za hali hiyo. Lakini kamati ya kitaifa inayohusika na wakimbizi wanahakikisha kuwa walipata taarifa hizo.

DRC inawapa hifadhi wakimbizi elfu 40 kutoka Burundi . Mwezi februari uliopita, warudi hao waliopewa hifadhi mashariki mwa nchi hiyo kubwa ya Afrika ya kati inayokabiliwa na usalama mdogo kwa takriban miaka 30 , walionyeshwa kwa baba mtakatifu François ambaye aliwapokea wahanga wa uhalifu unaofanyika mashariki mwa Kongo .

Previous Beni : zaidi ya watu 70 wauwawa katika kipindi cha siku 6
Next Goma : several private media deprived of access to information

About author

You might also like

Refugees

Nyarugusu (Tanzania) : all cell leaders sacked

The decision is from the Ministry of the Interior, in charge of refugees. It was implemented by the president of the camp. The measure was decried by Burundian refugees settled

Refugees

Mahama (Rwanda): a worrying lack of hygiene

Refugees in Mahama camp fear the infection of diseases linked to lack of hygiene. The reason is that clogged public toilets take long to be emptied. Camp sanitation officials are

Refugees

Nyarugusu : a refugee sentenced to 20 years for rape

A refugee from the Nyarugusu refugee camp located in northwestern Tanzania was recently sentenced to 20 years of criminal imprisonment, announced on December 17, Philemon Makungu, the police commander in