Beni : zaidi ya watu 70 wauwawa katika kipindi cha siku 6

Beni : zaidi ya watu 70 wauwawa katika kipindi cha siku 6

Zaidi ya watu 70 waliuwawa katika kipindi cha siku sita zilizopita katika wilaya ya Beni , Kivu kaskazini katika vijiji mbali mbali mashariki mwa DRC. Waliotekeleza mauwaji hayo ni waasi wa Uganda wa ADF. Watu hao waliuwawa katika vijiji vya Mukondi, Maghusa, na Kilindera. HABARI SOS Médias Burundi

Eneo la Mukondi, waasi waliuwa angalau wananchi 43 na kuwapeleka msituni wengine wengi. Eneo la Maghusa na Kilindera, waasi waliwakata vichwa wananchi zaidi ya 30.

Wengine wengi walitekwa nyara na nyumba zao kuchomwa moto.

” Licha ya mauwaji hayo yanayorudia, na idadi ya waliouwawa kuzidi kuongezeka, serikali bado imesalia kimya”, alibaini mkaazi mmoja.

” Hakuna ujumbe wa pole kwa wananchi au kulaani mauwaji hayo”. Hali hiyo inasababisha wasi wasi kwa wakaazi wengi wa eneo hilo ambao hawaelewi mwenendo huo ambao wengi wanadai kuwa ” ni udhaifu wa serikali “.

Mashirika ya kiraia katika wilaya ya Beni yaligundua kuwa ” maovu yanazidi kuongezeka katika eneo hilo licha ya ziara ya waziri wa ulinzi katika mji wa Goma na Ituri katika ukanda huo “.

” Waziri hakutumia fursa hiyo ya kwenda katika eneo hilo na kuleta suhulu la kuduma kwa sababu uwepo wa waasi unazidi kusikika katika vijiji mbali mbali, analaani muwakilishi wa mashirika ya kiraia ya ndani.

Wananchi wanaendelea kuunga mkono jeshi lao na wanapendekeza operesheni za pamoja kati ya jeshi la Kongo na Uganda ziweze kuendelea kwenye ardhi yote ya wilaya ya Beni.

Ifahamishe kuwa kati ya walioathiria, kuna watoto, akinamama pamoja na watu wenye umri mkubwa.

Previous Fizi : mapigano kati ya kundi la Mai Mai na Twirwaneho
Next Lusenda-Mulongwe : njaa yapiga hodi katika kambi za wakimbizi kutoka Burundi