Mzozo mashariki mwa Kongo : Rwanda na Tanzania zawapokea wakimbizi wapya kutoka Kongo zaidi ya elfu nane

Mzozo mashariki mwa Kongo : Rwanda na Tanzania zawapokea wakimbizi wapya kutoka Kongo zaidi ya elfu nane

Nchini Rwanda, HCR inayotoa takwimu hizo inaeleza kuwa mahitaji ya kibinadamu yanaongezeka wakati idadi ya wakimbizi kutoka Kongo wanaokimbilia nchini Rwanda kwa ajili ya usalama wao inapozidi kuongezeka. Katika miezi mitatu iliyopita, wakimbizi hao wanakadiriwa kuwa 6000. Nchini Tanzania, viongozi wa nchi hiyo wanafahamisha kuwa waliwapokea wakimbizi zaidi ya 2600 kutoka Kongo tangu tarehe 10 machi. Kati yao kuna pia waliokuwa wakimbizi zamani. HABARI SOS Médias Burundi

RWANDA

Ma elfu ya wananchi wa Kongo walilazimika kutoroka makaazi yao kutokana na mapigano yanayoendelea mashariki mwa jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo ( DRC). Ma mia kati yao wanaendelea kuwasili nchini Rwanda kila wiki kwa ajili ya usalama wao kwa mjibu wa HCR inayowahudumia.

Idadi kubwa kati yao walihifadhiwa kwanza katika kituo cha muda cha Kijote wiki moja kabla ya kuhamishwa katika kambi ya mapokezi ya Nkamira ndani ya kanda ya Rubavu kwenye mpaka na Goma mji mkuu wa mkoa wa kivu kaskazini.

” Tulikimbia kutokana na mapigano. Majirani walikuwa wakiuwawa. Ilikuwa sio rahisi kufika hapa, kulikuwa na vituo vingi vya ukaguzi pamoja na waasi njiani. Mara nyingi waliwapeleka watu kwenye vituo kwa ajili ya kukaguliwa lakini tulipata bahati. Tuliweza kupita”, wakimbizi walitoa ushuhuda huo kwa HCR.

” Tulikuja nchini Rwanda sababu kuna usalama zaidi ya kwetu. Tulileta nguo ambazo tulikuwa tunavaa tu. Haiwezekani kubeba mkoba wakati kuna mtu anayekimbia nyuma yako, walizidi kusema .

Ongezeko la vurugu eneo la mashariki mwa RDC lililazimisha zaidi ya watu wapya 5.400 kuomba hifadhi nchini Rwanda katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita. Wapya wanaoingia hupewa hifadhi katika kambi ya mapokezi ya Nkamira, wakati waliowasili kabla ya tarehe 12 januari wakiwa walipelekwa katika kambi ya wakimbizi ya Mahama mashariki mwa Rwanda.

Mbali na wapya wanaoingia, Rwanda inawapa hifadhi wakimbizi kutoka Kongo zaidi ya elfu 72.000. Walipewa hifadhi katika kambi tano nchini humo. Baadhi yao wanaishi kambini kwa zaidi ya miongo mitatu.

HCR pamoja na mashirikia mengine ya umoja wa mataifa, mashirikia ya kihisani pamoja na serikali ya Rwanda wanafanya kila liwezekanalo kuhakikisha maisha ya wakimbizi kutoka Kongo yanakuwa mazuri kwenye ardhi ya Rwanda .

Licha ya juhudi kwa ajili ya kuhudumia mahitaji ya wakimbizi yanayozidi kuongezeka, haki ya kupewa mahitaji ya msingi kama kupata makaazi ili kuepuka msongamano, madawa , ghala za vyakula magodoro ……bado ni nadra kupatikana, HCR inalalamika.

TANZANIA

Nchini Tanzania, viongozi wa nchi hiyo walifamisha kuwa zaidi ya raia wa Kongo 2600 waliomba hifadhi ya ukimbizini nchini humo tangu tarehe 10 machi.

Wadau wa kikanda wa naowahudumia wakimbizi katika mkoa wa Kigoma Kaskazini magharibi mwa Tanzania walitoa takwimu hizo jumatano hii katika mkutano na wandishi wa habari wa eneo hilo.

” Kwa ushirikiano na HCR, tunawapokea angalau watu 300 raia wa Kongo wanaomba hifadhi kila siku. Takriban wote ni wenye asili ya eneo la Kivu. Ni kutoka miji ya Beni na Goma” alifahamisha Noashoni Joel Makundi.

Hadi wakati huu, 600 kati yao walielekezwa katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu ambayo inawapa hifadhi wakimbizi kutoka Burundi na Kongo zaidi ya laki moja na elfu 35.

” Mapigano yanaendelea kati ya waasi wa M23 na jeshi la FARDC ( jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo). Ndugu zetu wanauwawa na sisi tulikuwa chini ya vitisho, ndio sababu tulilazimika kukimbia ” raia hao wa Kongo waliopokelewa Kigoma, walitoa ushuhuda huo.

Baadhi wanarejea tena kuomba hifadhi ya ukimbizi baada ya kurudi makwao na viongozi wa Tanzania wanafahamu hali hiyo.

” Ni kwa sababu hiyo tunalazimika kufanya uchunguzi wa kina kabla ya kuwatuma katika kambi ya Nyarugusu”, alifahamisha gavana wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye.

Raia wa Kongo waliopokelewa na Tanzania, walipewa hifadhi ndani ya kibanda kimoja kwenye makao makuu ya Kigoma. Kwa mjibu wa takwimu za mwisho za HCR, Tanzania inawapa hifadhi wakimbizi kutoka Kongo zaidi ya elfu 80.

Wakaazi wa eneo la mashariki mwa nchi hiyo kubwa ya Afrika ya kati, wanaendelea kukimbia nchi yao wakati zikiendelea kujengwa kambi za wakimbizi wa ndani eneo hilo.

Kwa mjibu wa ofisi ya mratibu wa maswala ya misaada ya kiutu OCHA, karibu watu elfu 530 walitoroka makaazi yao kutokana na mapigano na usalama mdogo katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita ndani ya mkoa wa Kivu Kaskazini.

Previous Crisis in Eastern Congo : Rwanda and Tanzania receive more than 8,000 new Congolese refugees
Next Goma: vyombo vya habari vingi vyanyimwa haki ya kupata habari