Goma: vyombo vya habari vingi vyanyimwa haki ya kupata habari

Goma: vyombo vya habari vingi vyanyimwa haki ya kupata habari

Vyombo vya habari vya ndani na kimataifa vinadai kubaguliwa katika kuripoti matukio yanayojiri kwa wakati huu ndani ya nchi na katika kanda. Wandishi wa habari wanapinga hali ambapo matukio yanayoweza kumulikwa na vyombo vya habari na kutoa taarifa kwa wananchi hufanyika faraghani. Wanaomba ihakikishwe haki ya kupata habari. HABARI SOS Médias Burundi

Taasisi zimeamuru kuchagua vyombo vya habari vinavyotangaza habari kama zinavyopendekeza taasisi hizo badala ya kuheshimu matukio” walilaani wandishi wa habari.

” Vikao na wandishi wa habari vinavyoandaliwa na mashirika mbali mbali ya ndani na kimataifa huangaziwa na vyombo vya habari vilivyochaguliwa na kuzuia vingine “, alitoa ushuhuda huo mwandishi wa habari wa ndani.

Kwa mfano mkutano na wandishi wa habari ulioandaliwa na ujumbe wa baraza la usalama la umoja wa mataifa mjini Goma mwishoni mwa wekendi iliyopita, uliibuwa maswala mengi.

Idadi kubwa ya vyombo vya habari hawakupata haki ya kuripoti juu ya mkutano huo.

” Umoja wa mataifa ulitayarisha orodha ya wandishi wa habari badala ya vyombo vya habari. Ni hivyo basi, idadi kubwa ya wandishi wa habari hawakualikwa katika mkutano huo. Mkutano huo ulikuwa na lengo la kukadiria hali ya usalama katika eneo hilo la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo na kutangaza suluhu pamoja na viongozi wa Kinshasa, Monusco na kikosi cha nchi za jumuiya ya Afrika mashariki ambacho jukumu lake ni kurejesha utulivu katika mkoa wa Kivu kaskazini”, alifahamisha mwandishi wa habari mmoja .

Kati ya vyombo vya habari na wandishi ambao hawakupata haki ya kuhudhuria mkutano huo ni pamoja na Sauti ya Amerika , Digital Kongo , les Volcans news , le Renouveau.NET, Kivumorningpost, actualité.Cd, Congo check na vingine”, alifahamisha mwandishi wa habari mwingine kati ya waliobaguliwa.

Kati ya wandishi wa habari waliopata mualiko, walikuwemo hata wale ambao hawako tena kwenye taaluma hiyo. Walipata mualiko kutokana na kujuana na baadhi ya maafisa wa Monusco. Wengine walikuwa wandishi wa habari lakini wasiofanyia kazi vyombo vya habari vilivyo kuwa kwenye orodha” alibaini mwandishi wa habari ambaye alishiriki katika mkutano huo.

Baadhi ya mashirika ya kiraia yalilalamika pia kwa kile walisema kuacha kupokelewa na ujumbe huo wa umoja wa mataifa.

” Umoja wa mataifa haukupendelea kila kitu kiwa dhahiri, na ni kwa sababu baadhi ya wananchi wa habari hawakualikwa katika mkutano.

Tuko katika serikali ya haki, serikali ambayo kila mtu ana uhuru wa kujieleza na kutoa maoni yake kuhusu yanayotokea ndani ya nchi yake ” , alisisitiza mwanaharakati wa mashirika ya kiraia eneo hilo.

Wandishi wa habari wamekuwa wakikabiliwa na vitisho kutoka kwa baadhi ya viongozi wa Kongo hususan linapofika swali au kutangaza udhaifu wa jeshi la Kongo kwenye uwanja mapambano.

Kwa mjibu wa shirika la wandishi wa habari ambao wako hatarini (JED), na shirika kwa ajili ya kutetea haki za wandishi nchini DRC, angalau asilimia 65 ya wandishi wa habari waliwahi kukamatwa na badaye kuachiwa huru na viongozi wa Kongo kwa tuhuma ya kuwapa fursa ya kuongea waasi katika eneo hilo la Afrika ya kati hususan Kivu kaskazini ambapo jeshi la taifa linapambana na kundi la M23.

Wandishi wa habari wengine waliuwawa katika maeneo ya vita na hali hiyo kusahawulika .

Previous Mzozo mashariki mwa Kongo : Rwanda na Tanzania zawapokea wakimbizi wapya kutoka Kongo zaidi ya elfu nane
Next Goma: the oil tankers' association goes on a strike