Ituri: angalau wananchi 28 waliuwawa katika mashambulizi ya waasi

Ituri: angalau wananchi 28 waliuwawa katika mashambulizi ya waasi

Jumapili iliyopita, waasi wa kundi la silaha la CODECO (shirikisho kwa ajili ya maendeleo ya Kongo) walifanya mashambulizi katika maeneo mbali mbali ya mkoa wa Ituri mashariki mwa DRC. Vyanzo vya ndani vinasema raia 28 waliuwawa, mali na madawa vikaibiwa. Mashirika ya kiraia ya ndani yanapongeza vikosi vya usalama kwa kuingilia kati mapema, lakini wanaomba taasisi hiyo kuongeza juhudi. HABARI SOS Médias Burundi

Mashambulizi hayo yalilenga vijiji na maeneo ya Bahema-kaskazini ndani ya wilaya ya Djugu, kwa mjibu wa mashahidi.

” Waasi wengi waliingia ndani ya soko la kijiji cha Nzengele tarafa ya Walendu-Binti. Walibomoa vibanda na maduka eneo hilo na kuwauwa watu 16″, mashahidi wanasema.

Wakati huo huo, waasi wengine wa kundi hilo walilenga ofisi ya uongozi wa Bahema-kaskazini eneo la Blukwa. Eneo hilo waliwauwa watu watano na kujeruhi mtu mwingine, pamoja na kuiba bidhaa. ilikuwa majira ya saa kumi na mbili , kwa mjibu wa vyanzo vyetu.

Kama vile hiyo haikutosha, kundi jingine lilielekea katika eneo la Walendu-Binti na Tatchi. Walishambulia parokia ya kanisa katoliki ya Drodro pamoja na hospitali kuu ya eneo hilo”, wakaazi wanalaani uporaji wa madawa na vifaa vya hospali.

Mashirika ya kiraia yanaripoti kuwa waasi walipita katika kijiji cha Largu ambako waliwauwa wananchi saba.
Matokeo ya mashambulizi ya jumapili ni watu 28 kuuwawa katika eneo la Bahema-kaskazini.

Mashambulizi hayo yalidaiwa kutekelezwa na CODECO wakati ambapo kundi hilo hivi karibuni lilishiriki katika mazungumzo ya Nairobi (Kenya) ambapo walisaini mkataba wa amani mkoa wa Ituri.

Previous Rumonge: rais Neva atoa tahadhari kwa naibu mkuu wa chama cha CNDD-FDD na kuahidi kumupeleka mahakamani gavana wa zamani
Next Mahama (Rwanda): the health component entrusted to “Save the children”

About author

You might also like

Refugees

Kakuma (Kenya): two Burundian refugees killed

Two Burundian refugees have been killed and several others injured, in a week, at Kakuma camp in northwestern Kenya. Nearly all the victims were ambushed allegedly by the South Sudanese

Security

Ntega: a young man who assaulted his wife was killed by a policeman

This young man, in his twenties, was killed by a police officer at nightfall on Monday. The information is confirmed by the local administration, which explains that the victim was

Human Rights

Tanzania : more than 100 CNL members seeking asylum

More than a hundred Burundians, members of the opposition CNL party, mainly from the Gitega, Ruyigi and Makamba provinces, fled the country at the end of last week. They fled