Rumonge: rais Neva atoa tahadhari kwa naibu mkuu wa chama cha CNDD-FDD na kuahidi kumupeleka mahakamani gavana wa zamani

Rumonge: rais Neva atoa tahadhari kwa naibu mkuu wa chama cha CNDD-FDD na kuahidi kumupeleka mahakamani gavana wa zamani

Rais Ndayishimiye ametoa tahadhari kwa naibu katibu wa chama tawala katika mkoa wa Rumonge (Kusini-magharibi mwa Burundi). Anamutuhumu kuvuruga uchaguzi wa mkuu wa tarafa mpya. Ametoa muda wa wiki moja kwa mabaraza ya tarafa za Rumonge, Bugarama, na Buyengero kuwa wamewachagua wakuu wapya wa matarafa hayo. Rais Neva ameahidi pia ” kumupeleka mahamani gavana wa zamani wa mkoa ” Consolateur Nitunga ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa mshahuri kwenye ubalozi wa Burundi mjini Kinshasa makao makuu ya Kongo. HABARI SOS Medias Burundi

Naibu katibu wa chama tawala cha CNDD-FDD katika mkoa wa Rumonge ameondolewa nje ya jukwa la heshma na wafanyakazi kwenye ofisi ya rais wakati rais Ndayishimiye akihutubia kwa dakika kadhaa.

Rais wa jamuhuri ya Burundi amemtaka kuacha kujihusisha na uchaguzi wa wakuu watatu wa tarafa. Ni wakuu wa tarafa ambao watachukuwa nafasi za wale wanaozuiliwa katika gereza kuu la Mpimba ( jiji kuu la biashara) kwa kosa la wizi wa mabati na simenti vilivyotolewa na ofisi ya rais kwa ajili ya ujenzi wa shule.

Kulingana na chanzo eneo la tukio tarafani Bugarama, Clément Ndikumana huenda alizuia uchaguzi wa mkuu mpya wa tarafa ya Bugarama. Anataka mjumbe wa familia yake aweze kuhudhuria vikao vya baraza la tarafa na kuchaguliwa kama mkuu wa tarafa.

” Hayo ni wakati wadhifa wa mkuu wa tarafa ya Bugarama utapewa mshahuri mwingine wa kabila la watutsi kama ilivyopangwa na sheria ya uchaguzi ya 2020″ , chanzo karibu na faili hiyo kinasisitiza.

Wiki iliyopita, uchaguzi wa wakuu hao watatu wa tarafa za Rumonge Bugarama na Buyengero uliahirishwa.

Mbali na kuahirisha uchaguzi, chama cha CNDD-FDD kinatuhumiwa kukiuka sheria ya tarafa. Chama cha upinzani cha CNL kilipinga kushiriki katika uchaguzi huo na kudai sheria juu ya uchaguzi iheshimiwe.

Mwishoni mwa novemba 2020, wakuu watatu wa tarafa; Jérémie Bizimana mkuu wa tarafa ya Rumonge, Charles Karorero mkuu wa tarafa ya Bugarama pamoja na Gratien Nduwayo, mkuu wa tarafa ya Buyengero walisimamishwa. Wanatuhumiwa kufanya ubadilifu na wizi wa vifaa vya ujenzi wa shule vilivyotolewa na ofisi ya rais wa jamuhuri ya Burundi.
Wakuu wa tarafa hao watatu, wanazuiliwa katika gereza kuu la Mpimba jijini Bujumbura.

Gavana wa zamani kuhusishwa katika kesi hiyo

Rais Neva aliahidi kumurejesha nyumbani gavana wa zamani wa mkoa wa Rumonge Consolateur Nitunga ambaye hivi karibuni aliteuliwa kama mshahuri kwenye ubalozi wa Burundi mjini Kinshasa.

Ni aibu kusikia mkuu wa tarafa akikubali kuwa alifanya ubadilifu wa mali ya umma lakini hapo hapo, akiomba mwendeshamashtaka kuacha kumufatilia. Nina bahati. Waliniambia kuwa ni gavana wa zamani aliyetoa amri ya kufanya hivyo. Nitamuitisha ili aweze kujibu mashtaka dhidi yake wakiwa pamoja. Muda wa ma mapumziko tayari umeisha. Faili ziko tayari. Atafikishwa mahakamani”, ametangaza rais wa Burundi mkoani Rumonge. Alikuwa akimutambulisha gavana mpya kwa wananchi wa eneo hilo.

Raia Ndayishimiye alidai kuwa litakuwa jambo la kushangaza iwapo gavana wa zamani Consolateur Nitunga hakuhusika na wizi wa vifaa hivyo vya kujenga shule ndani ya mkoa aliyekuwa akiongoza.

Matamshi ya raia Ndayishimiye yamesikika kama bomu kwa wanaounga mkono mkuu wa tarafa Jérémie Bizimana anaendelea kugonga kwenye milango ya wanasiasa wa nchi hii kwa ajili kumuondolea mashtaka na hivyo aweze kuwaachiliwa huru na kuendelea kuongoza tarafa ya Rumonge.

Kwa mjibu wa chanzo cha ndani ya ofisi ya mkuu wa tarafa ya Rumonge, mkuu wa tarafa aliyesimamishwa Jérémie Bizimana huenda alikanusha mashtaka dhidi yake kuhusiana na ubadilifu akisahawu kuwa yeye binafsi alituma ujumbe wa sauti kwa mwendeshamashtaka wa jamuhuri mkoani Rumonge akimuomba kumukingia kifua.

Previous RDC: jamii ya Banyamulenge wanahofia mauwaji ya kikabila, wanatoa malalamiko kwa EAC
Next Ituri: angalau wananchi 28 waliuwawa katika mashambulizi ya waasi