RDC: jamii ya Banyamulenge wanahofia mauwaji ya kikabila, wanatoa malalamiko kwa EAC

RDC: jamii ya Banyamulenge wanahofia mauwaji ya kikabila, wanatoa malalamiko kwa EAC

Madiwani pamoja na viongozi wa jamii ya Banyamulenge eneo la Minembwe (mkoa wa kivu-kusini, mashariki mwa DRC) walimuandikia barua rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye kama mwenyekiti wa EAC (jumuiya ya afrika mashariki). Wanamutahadharisha kuhusu ” mpango wa mauwaji ya kikabila yanayowalenga wajumbe wa jamii ya Banyamulenge. Rais Ndayishimiye hajatoa majibu. HABARI SOS Médias Burundi

Katika barua hiyo ambapo nakala ilipewa ma rais wote wa nchi za EAC mbali na rais wa Sudani kusini, madiwani wanalaani mpango wa ” mauwaji ya kikabila ” dhidi ya jamii yao.

Wanaelezea operesheni za jeshi la FARDC (jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo) kwa ushirikiano na wanajeshi wa Burundi na kundi la Mai-Mai.

Tarehe 29, 15, na 7 disemba 2022 pamoja pia na 9 oktoba mwaka huo, siku hizo zinatajwa na madiwani Banyamulenge kama mifano ya utekelezwaji wa mpango waliotaja kama ” mauwaji ya kikabila”.

Katika nyakati hizo, wajumbe wa jamii ya Banyamulenge waliuwawa.

[…] mpango wa mauwaji ya kikabila uliandaliwa na jeshi la FARDC kwa ushirikiano na majeshi ya Burundi eneo la Minembwe”, madiwani wanatuhumu.

Wanataja majina ya wahanga na kudai kuwa ni maafisa wa jeshi la Kongo wanaowajibika katika mauwaji hayo.

Rais wa Burundi ambaye sasa ni mwenyekiti wa EAC hajatoa majibu. Lakini jamii ya Banyamulenge wanamuomba ” kuchukuwa tahadhari wakati ambapo wanajeshi kutoka nchi yake wakiunga mkono mpango wa mauwaji ya kikabila kuliko kufanya kazi kwa ushirikiano na kikosi cha kikanda cha EAC kwa ajili ya kulinda wananchi na mali zake pasina kubagua rangi au kabila.

Barua hiyo ilisainiwa na viongozi wa kijadi 13 wa tarafa ya Minembwe. Nakala ilipewa rais Uhuru Kenyatta rais mstaafu wa Kenya na mpatanishi katika mgogoro nchini Kongo. Ingawa jamii ya Banyamulenge wanatuhumu jeshi la FARDC kuandaa mauwaji ya kikabila, naibu mkuu wa jeshi la Kongo anayehusika na operesheni, alifahamisha jumatano tarehe 4 januari 2022 kuwa “[…] ulinzi na udhibiti wa ardhi ya Kongo, ulinzi wa wananchi na mali zao, ni msingi wa jukumu la jeshi la FARDC “.Jemedali Chiko Tshitambwe Jérôme alikuwa ziarani eneo la Minembwe katika wilaya ya Fizi. Alielekea eneo hilo kwa lengo na kufuatia operesheni ya pamoja kati ya jeshi la Burundi na Kongo dhidi ya kundi la wapiganaji vijana wa jamii ya Banyamulenge la Twirwaneho.

” wanajeshi wa Burundi walikuja kutuunga mkono kwa ajili ya kutokomeza makundi yote ya silaha ya nje na ndani ya nchi, alizidi kusema.

Banyamulenge ni jamii ya wananchi wa Kongo ambao ni wafugaji. Wanachukuliwa na jamii zingine kama raia wa Rwanda kwa sababu wanatumia lugha inayotaka kufanana na Kinyarwanda.

Wanadai kuwa wamenyanyaswa kwa miaka mingi. Tangu kuibuka tena kwa kundi la M23 mwishoni mwa mwaka wa 2021 kundi linaloundwa na jamii ya watutsi, jamii ya watu wanaozungumza lugha ya Kinyarwanda wanaoishi nchi DRC wanatuhumiwa pamoja na nchi ya Rwanda kuunga mkono waasi hao”. UN inalaani kauli za chuki zinazolenga jamii hiyo na kushawishi wananchi kuwashambulia. UN inaomba viongozi wa Kongo ” kusimamisha mara moja matamshi hayo”. Lakini rais Paul Kagame anaona kuwa ” jamii ya kimataifa inasifu amani ya mdomoni”.

Angalau wananchi wa Kongo 1700 wanaotumia lugha ya Kinyarwanda wengi wao wakiwa wenye asili ya mkoa wa Kivu kaskazini walikimbilia nchini Rwanda wiki kadhaa zilizopita. Wanadai kukimbia mateso wanayofanyiwa baada ya kufananishwa na maaduwi wa Kongo na nje.

Rais Kagame hivi karibuni alihakikisha kuwa nchi yake inawapa hifadhi zaidi ya wakimbizi elfu 70 kutoka Kongo, wajumbe wa jamii ya wanaotumia lugha ya Kinyarwanda na kulaani kuwa “[…] lakini jamii ya kimataifa inadai kuwa watu hao hawapo…. Inaonekana mpango ni watu hao kusalia nchini Rwanda, msimamo ambao utawasaidia kujitetea juu ya uongo wao kwamba watu hao ni raia wa Rwanda ambao wanatakiwa kufukuzwa” . Kwa mjibu wa Kagame, hilo ni tatizo la kimataifa linalotakiwa suluhisho la kimataifa”.

Raia Félix Tshisekedi aliwaomba raia wa Kongo kujizuia kufanya vitendo vya chuki dhidi ya raia wa Rwanda huku akidai kuwa ” ni utawala wa Rwanda ukisimamiwa na Rais Paul Kagame ambao ni aduwi wa jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo “.

Kwa mjibu rais wa nchi hiyo kubwa ya afrika ya kati ambayo sehemu yake inakabiliwa na usalama mdogo kwa zaidi ya miongo mitatu. Hali hiyo ilisababishwa na makundi ya silaha ya ndani na nje ya nchi ambapo wakuu wa jeshi na viongozi serikalini walituhumu kushirikiana na waasi “, ” Raia wa Rwanda wanahitaji msaada wetu sababu walinyanyaswa. Wanahitaji mchango wetu ili waweze kujikwamua na kuwa huru. Wanahitaji ushirikiano wetu ili kutenganisha nchi na afrika mbali na aina hiyo ya viongozi wanaotumia mbinu za miaka ya 60 na 70 “.

Previous Burundi: mkuu wa CNIDH kuendelea kuongoza tume hiyo, wanaharakati wana matumaini kwake
Next Rumonge: rais Neva atoa tahadhari kwa naibu mkuu wa chama cha CNDD-FDD na kuahidi kumupeleka mahakamani gavana wa zamani

About author

You might also like

Politic

Rutana: an influential CNDD-FDD activist sentenced to one year in prison

Nestor Butisi Nibigira, a shopkeeper and influential CNDD-FDD activist in the commune of Giharo received a one-year prison sentence and pay a fine of 2.5 million Burundian francs. The decision

Politic

Gitega : a short arrest of members of the CNL party that leaves questions

Methuselah Nijimbere, Pascal Nyambere and Nestor Ciza were arrested Thursday early in the afternoon by Imbonerakure (members of the CNDD-FDD youth league) and the police then taken to the dungeons

Society

Burundi: HRW demands the release of Floriane Irangabiye

Human Rights Watch believes that the conviction of the Burundian journalist breaches the right to freedom of expression. It says that authorities should release Floriane Irangabiye and end what they