Burundi: mkuu wa CNIDH kuendelea kuongoza tume hiyo, wanaharakati wana matumaini kwake

Burundi: mkuu wa CNIDH kuendelea kuongoza tume hiyo, wanaharakati wana matumaini kwake

Sixte Vigny Nimuraba aliidhinishwa kuendelea kuongoza CNIDH (tume ya kitaifa ya haki za binadamu) kwa muhula wa miaka minne.Bwana Nimuraba aliahidi kushirikisha na wadau wote kwa ajili ya kupata nchi ya Burundi ambako haki za kila mwananchi zinaheshimiwa. Shirika la Iteka, shirika la zamani kabisa la kutetea haki za binadamu nchini Burundi linasema kuwa na uaminifu kwake. HABARI SOS Médias Burundi

Ni bunge la taifa lililomuidhinisha Sixte Vigny Nimuraba kuendelea kuongoza tume hiyo. Walioidhinishwa kuendelea kwa muhula mwingine wa miaka minne, ni Jacques Nshimirimana mjumbe wa tume hiyo pamoja na Consolatte Hitimana katibu wa tume hiyo ambaye hadi sasa alikuwa naibu kiongozi wa CNIDH. Anaclet Nzohabonayo ni naibu kiongozi wa kamati hiyo wakati ambapo Anésie Mfatiyimana aliingizwa ndani ya tume hiyo ya haki za binadamu nchini Burundi kama mjumbe pamoja pia na naibu kiongozi.

Kiongozi huyo anayeendelea, alipitishwa kwa 100% yaani kwa kura 116 kwa jumla ya watu 116 walioshiriki, dalili kwamba watu wanaamini kazi ya tume hiyo kwa mjibu wa wahusika.

[…] hilo linanipa moyo wa kuongeza mipango pamoja na juhudi katika kulinda haki za binadamu lakini pia na kuendelea kuimarisha ushirikiano na taasisi zingine za serikali na mashirika mengine yanayohudumu katika sekta ya haki za binadamu nchini Burundi, aliwahakikishia wandishi wa habari wa ndani Sixte Vingy Nimuraba baada ya kikao cha kumuidhinisha.

Kwa mjibu wa bwana Nimuraba, akiwa hata mtu mmoja ambaye haki zake zimekiukwa ni masikitiko”.

SOS Médias Burundi ilitaka kufahumu maoni ya wanaharakati wa haki za binadamu kukusu kuendelea kwake kuongoza tume hiyo. Idadi kuwa hawakuwa karibu ili kijieleza. Lakini kiongozi wa shirika la zamani kabisa la kutetea haki za binadamu alizungumza. Anschair Nikoyagize alisema kuridhika.

” Shirika la Iteka tunaridhishwa na uteuzi wa Daktari Vingy wa kuendelea kuongoza sababu alifanya kazi tofauti na mtangulizi wake. Muhala wake na ule wa mtangulizi wake ni tofauti”, alijipongeza Nikoyagize.

Na kuendelea kuwa ” aliwahi kusogelea mashirika ya kutetea haki za binadamu yaliyotoroka nchi likiwemo la Iteka. Tayari tulifanya mkutano kwa njia ya video. Kwa hiyo, natumai kuwa ataweza kufika ikizingatiwa utashi wake na nia yake ya kushirikiana na wadau wote, tuna matumaini kwake”.

Na kutoa ushuhuda.

” Mnakumbuka kuwa alitishiwa na spika wa baraza la bunge mara kadhaa. Hiyo ni dalili kuwa anawajibika, alifanya kile ambacho serikali ya sasa na bunge wanataka kuficha jamii ya kimataifa. Ni kweli ripoti zake hazijumilishi matukio yote wakati ambapo uwezo upo…..lakini anafanya kazi pia katika mazingira magumu kwa sababu anatishiwa na ma jemedali, watu hao ambao hawataki sekta ya haki za binadamu isonge mbele”.

Kwa jumla watu 46 walikuwa wamewasilisha faili zao lakini 15 peke ndio walichukuliwa kwa ajili ya kuwasilishwa katika bunge la taifa jumatatu hii. Nafasi tano zilikuwepo. Nafasi 9 wa wajumbe wa kabila la wahutu, na 6 za Watutsi. Wajumbe watatu wa kamati kuu waliidhinishwa akiwemo mmoja wa jamii ya watutsi pamoja na ma kamishna wawili akiwemo kutoka Kabila la watutsi pia. Hayo ni kulingana na sheria inayopanga shughuli za CNIDH ya januari 2011.

Majina hayo yaliyoidhinishwa na bunge yatatumwa kwa rais ambaye ataidhinisha uteuzi wao kupitia sheria ya kirais.

Sixte Vingy Nimuraba alieyeidhinishwa kuendelea kuongoza tume hiyo ya CNIDH aliwajibika hadi tume hiyo ikarudishwa kwenye kiwango cha A. Baraza la haki za binadamu la umoja wa mataifa lilichukuwa hatua hiyo mwezi juni 2021 na CNIDH ikarudi kwenye kiwango cha A.

Taasisi hiyo ya Burundi ilishushwa katika mwaka wa 2018 kwa sababu ya kufumbia macho ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. UN inaona kuwa kuna hatua iliyopigwa kuelekea njia nzuri.

Previous Bubanza: demobilized soldiers concerned about the lack of law governing them
Next RDC: jamii ya Banyamulenge wanahofia mauwaji ya kikabila, wanatoa malalamiko kwa EAC