Burundi : ukosefu wa mafuta ya gari watangazwa kwa mara nyingine

Burundi : ukosefu wa mafuta ya gari watangazwa kwa mara nyingine

Ni ukosefu wa mafuta kwa mara nyingine tena kulingana na wasafiri. Kwenye vituo vya mafuta, milolongo mirefu ya magari imeshuhudiwa jumatatu hii pasina matumaini ya kupata bidhaa hiyo. Badala yake, kwenye soko la kienyeji hasa katika kata ya Buyenzi ndani ya jiji la Bujumbura, mafuta yanapatikana lakini lita moja hupatikana na bei ya franka 5000 sarafu za Burundi. HABARI SOS Médias Burundi

Bujumbura

Kusini mwa jiji kuu la kibiashara, eneo la Kanyosha, vituo vya mafuta vimefungwa.

Kwenye kituo karibu na Brarudi ( kiwango cha kutengeneza vinywaji), mlolongo wa magari yanasubiri lakini waendesha magari hayo hawana matumaini.

” Tunasubiri lakini hatuna matumaini sababu hatujuwi iwapo kituo hichi kitapata au la ” analalamika dereva mmoja anayefanya kazi ya uchukuzi.

Kwenye kituo karibu na soko maarufu kwa Sioni kaskazini mwa jiji, hakuna hata tonya moja ya mafuta aina ya Diesel au Petroli iliyopatikana.

Hali ni kama hiyo katika vituo vya mafuta vinavyopatikana pembeni ya barabara kuu Adolphe Nshimirimana.

” Tunapata tabu kutumika ” amelalamika dereva mmoja aliyekuwa eneo hilo.

Kulingana na taarifa zetu, vituo vine peke katika mji mkuu wa kiuchumi wote vilipewa mafuta aina ya petroli katika siku ya jumapili jioni.

Hata hivyo, baadhi ya waendesha magari walifahamisha kuwa mafuta hayo yalidumu muda mfinyu sana. Walitufahamisha kuwa mafuta hayo yalitolewa ndani ya vituo hivyo ili kupelekwa katika soko la kienyeji.

Jumatatu hii kwenye soko la kienyeji ndani ya kata ya Buyenzi, lita moja aina ya petroli au Essence limeuzwa zaidi ya franka elfu 5000 sarafu za Burundi na jerikani ya lita 20 bei yake ilikuwa laki moja kulingana na waendesha magari ya abiria ambao wanazidi kusema kuwa hawana chaguo jingine mbali ya kutafuta bidhaa hiyo kwenye soko la kienyeji.

” Hatuna njia nyingine. Tunatafutia eneo hilo ingawa bei ni kubwa. Tunalazimika kutumika ili tuweze kuhudumia familia zetu”, wanasema . Bei ya lita moja ya mafuta aina ya petroli kawaida ni franka 3250 safaru za Burundi.

Wakaazi wa jiji kuu la biashara wanaomba serikali itafute suluhu la kudumu kuhusu tatizo hilo la uhaba wa mafuta ya gari.

Bubanza

Katika mkoa wa Bubanza, (magharibi) waendesha pikipiki za abiria wanasema kuwa wanakabiliwa na tatizo kubwa katika kulisha familia zao. Kadiri ya kuchukuwa madeni sana, tunakabiliwa na hatari ya kuchukuliwa kama matapeli”, wanasema huku bei ya nauli ikiwa imepanda mara dufu.

Cibitoke

Abiria wengi jumanne hii hawakuweza kuwasili katika maeneo ambapo wametaka kuelekea.

” Ninamaliza muda wa saa tatu ndani ya maegesho haya. Siku yangu imeharibika ” , amelalamika mwanaume mmoja aliyekuwa kwenye makao makuu ya mkoa huo. Alikuwa na safari ya kuelekea katika mji mkuu wa kibiashara wa Bujumbura.

Dereva wa basi mmoja amedai kuwa ” hali hiyo itasababisha matatizo makubwa sababu idadi kubwa ya wanaume wanarudi nyumbani mikono mitupu”.

Kulingana na taarifa, ukosefu wa mafuta ya gari ndio chanzo cha mfumuko wa bei ya bidhaa za vyakula unaoshuhudiwa kwenye soko la vyakula na ndani ya maduka.

Hivi karibuni, rais wa nchi alifahamisha kuwa ” hana bomba la kuchotea dola pamoja na mafuta ya gari vinavyotafutwa “.

Hali inaweza kuwa mbaya zaidi katika nchi hiyo ndogo ya Afrika mashariki ambako hamna ghala la akiba la mafuta. Waziri wa nishati anayehusika na urasibu wa mafuta aliwambia wajumbe wa baraza la seneti kuwa ” Ghala zote za mafuta hazina bidhaa hiyo ikiwa ni Bujumbura au Gitega”.

Previous Gitega : watuhumiwa watano wa mapenzi ya jinsia moja wameachiwa huru kwa jumla ya wale 24 wanaozuiliwa jela
Next Bujumbura: the prosecutor to the Ntahangwa Court of Appeal and his substitute in jail