Nyarugusu (Tanzania) : zaidi ya wakimbizi mia moja wenye asili ya Burundi walazimishwa kurejea makwao kwa nguvu

Nyarugusu (Tanzania) : zaidi ya wakimbizi mia moja wenye asili ya Burundi walazimishwa kurejea makwao kwa nguvu

Kwa sababu ya kutokuwepo wakati wa sensa kwa ajili ya uhakikisho ya mwaka wa 2021, shirika linalowahudumia wakimbizi (HCR), liliondoa wakimbizi wenye uraia wa Burundi zaidi ya mia moja kwenye orodha ya wale wanastahili kupewa misaada. HABARI SOS Medias Burundi

Chanzo cha mkasa huo ni sensa nyingine ya kuthibitisha iliyofanyika “kwa kushitukiza” ndani ya kambi ya Nyarugusu mwaka wa 2021.

” Watu wengi hawakuwa kambini. Walikuwa katika miji ya Dar Es Salam , Kigoma na Mwanza kwa ajili ya kutafuta ajira. Wengine walikuwa kwenye vyuo vikuu mbali mbali kusoma huku wengine hususan wasichana wakiwa waliolewa na raia wa Tanzania” wakimbizi walitoa ushuhuda huo.

Lakini kuanzia mwaka uliopita, wengi kati yao walirejea kambini wakitegemea kuendelea kupata misaada kutoka HCR.

Lakini kwa mshangao mkubwa, walifahamishwa kuwa hawatambuliki tena kama wakimbizi.

” Ni jambo lisiloeleweka. Unaweza kupata mume au mke ambaye sio mkimbizi wakati ambapo watoto ni wakimbizi. Mjumbe wa familia anaweza kukosekana kwenye orodha wakati wa ndugu zake ma kaka na ma dada wakiwepo” wakimbizi wanaeleza.

Wahusika waliamuru kutoa malalamiko ambayo yalichukuwa zaidi ya mwaka mmoja. Lakini mwisho hayakukubaliwa, kama ilivyotangaza Danish Refugee Council ( DRC).

Hivyo, kulingana na shirika la DRC, hadhi ya ukimbizi inarejeshwa wakati muhusika anapojiorodhesha ili ” kurejea makwao kwa hiari “

” zaidi ya 50 kati yao walirejeshwa wiki hii na wiki iliyopita sababu walikuwa hawana chaguo jingine. Wengine wanasubiri kuchukuwa njia hiyo sababu hawapati tena msaada. Wanapopatwa na maradhi, hawatibiwi. Ndani ya kambi wanatafutwa kama wahalifu”. watu wa karibu yao wanalaani na kukosoa ” mpango wa ulioundwa kwa ushirikiano kati ya Tanzania na Burundi “.

” Tunahofia hata usalama wao ndani ya kambi sababu kuna wengine ambao bado wanaojificha hapa. Mara baada ya kuwasili nchini Burundi, wakipata tatizo lolote, HCR itaulizwa “, wanasisitiza huku wakiomba hatua hiyo isimamishwe bila starti lolote na hatua ya kurejea iweze kuwa hiari wakati wa kurejesha wakimbizi.

Kambi ya Nyarugusu ina zaidi ya wakimbizi wa Burundi elfu 50.

Previous Rwanda: Paul Kagame atangaza kugombea urais mwaka wa 2024
Next Kesi-Bunyoni: Waziri mkuu huyo wa zamani anachukizwa na hali ya kinyama ya kuwekwa kizuizini na kuomba aachiliwe kwa muda