Rwanda: Paul Kagame atangaza kugombea urais mwaka wa 2024

Rwanda: Paul Kagame atangaza kugombea urais mwaka wa 2024

Paul Kagame, rais wa Rwanda ameambia gazeti la Jeune Afrique kuwa atagombea muhula wa nne katika uchunguzi mkuu wa 2024. Ilikuwa katika toleo la tarehe 19 septemba 2023. Mwezi aprili iliyopita, marekebisho mengine mawili muhimu ya katiba kuhusu muda wa muhula yalipendekezwa bungeni. HABARI SOS Medias Burundi

Mwanaume huyo shujaa wa Kigali hakusita hata sekunde moja ili kujibu swali ambalo sio la kushangaza kwa mjibu wake.

” Hakika nitakuwa mgombea. Ninafurahishwa na uaminifu ambao raia wa Rwanda wanaweka kwangu. Nitawahudumia daima kadiri ya uwezo wangu”, alifahamisha Paul Kagame katika gazeti la Jeune Afrique.

Akiwa madarakani tangu mwaka 2000, bwana Kagame amekosoa vikali nchi za magharibi ” zinazomutuhumu ” kijing’anganiza madarakani “.

Majibu

Demokrasia ni nini? Nchi za magharibi zinaamrisha nchi zingine la kufanya ? Lakini wanakwenda kinyume na misingi yao, vipi tuwasikilize ? Amejiuliza mkuu huyo wa zamani wa kikundi cha waasi wa Rwanda.

Mwenyekiti huyo wa FPR chama tawala anaonekana kupuzia ukosoaji ambao hautachelewa kumiminika kutoka mahala pote hasa kutoka jamii ya kimataifa.

” Pole kwa nchi za magharibi, lakini yale ambayo wanafikiria sio tatizo letu. Siko tena yule anayekwenda sawa na maadili ya nchi za magharibi “, alizidi kusema.

Tangazo la jemedali Paul Kagame halikushangaza watu wengi wakati ambapo mwezi aprili iliyopita, alikuwa ameanza kuimarisha njia yake ya kuelekea uchaguzi mkuu wa agosti 2024.

Tunaweza kutaja rasimu ya kutaka kurekebisha katiba ambayo iliwasilishwa bungeni, mabaraza mawili yakiwa pamoja na waziri wa sheria na mwendeshamashataka mkuu Emmanuel Ugirashebuja.

Kati ya mapendekezo ya rais, kuchaguliwa na wabunge na wajumbe wa baraza la seneti, muhula wa rais kupunguzwa kutoka miaka 7 na kugeuka 5 na uchaguzi wa urais na bunge kufanyika kwa wakati mmoja.

Uwezekano wa kuungwa mkono.

Hata kama kampeni ya uchaguzi ikiwa bad o kuanza mwaka mmoja kabla ya uchaguzi, inaonekana kama ushindi umepatikana kabla.

Kwenye mitandao ya kijamii inayotumiwa na vijana na wasomi wa Rwanda , vuguvugu la wanaounga mkono Kagame tayari limeanza. ” TeamPK ” inafuatiliwa sana na kuongezwa kasi na watu maarufu kwenye mitandao nchini Rwanda ambao wanatoa sifa za rais Paul Kagame

Akiwa na miaka 65, rais Paul Kagame anaongoza nchi hiyo inayoendelea kwa kasi kwa mjibu wa rikodi ya Benki kuu ya dunia.

” Kufanya tangazo hilo kubwa linaloweka hatiani nchi kupitia chombo cha kimataifa, sio jambo la kubahatisha kwa mjibu wa kiongozi huyo mwenye ushawishi wa Kigali. Ana mazoea ya kufanya hivyo hasa kuhusu faili za uhusiano wa kidiplomasian kati ya Rwanda na Burundi,Uganda , na DRC. Ni kupitia gazeti la Jeune Afrique ambapo bwana Kagame alifichua siri kuhusu mbinu zilizotumiwa kumukamata na kumuachilia huru “, ameeleza Pierre Claver Niyonkuru , mwandishi wa habari mwenye asili ya Burundi ambaye aliishi nchini Rwanda.

” na vyombo vya ndani, vilichuluwa tu habari hiyo ambayo tayari ilitangazwa kwenye vituo vya kimataifa, hali ambayo jamii ya kimataifa inakosoa vikali na kuichukulia kama unyanyasaji dhidi ya vyombo vya habari “, alimalizia .

Previous Goma : miili ya watu zaidi ya arobaini yazikwa kwa amri ya serikali licha ya upinzani wa familia na mashirika ya kirai
Next Nyarugusu (Tanzania) : zaidi ya wakimbizi mia moja wenye asili ya Burundi walazimishwa kurejea makwao kwa nguvu