Buganda: kijana Imbonerakure auwawa na mwanajeshi
Kisa hicho kilitokea alhamisi hii kwenye transversale ya nne katika kijiji cha Nyamitanga mkoa wa Cibitoke (kaskazini-magharibi mwa Burundi). Mwanajeshi alimpiga risasi kijana Imbonerakure (mfuasi wa tawi la vijana la chama cha CNDD-FDD). Alifariki papo hapo. Muhusika wa mauwaji hayo alikamatwa. HABARI SOS Médias Burundi
Muathiriwa ni kijana mwanafunzi aliyekuwa akielekea kumalika masomo mwaka ujao. Kwa mjibu wa mashahidi, ilikuwa majira ya saa moja ambapo Lahay Roy Niyera aliuwawa.
” Alikuwa akijaribu kuondoa udongo katika barabara ili kuruhusu nenda rudi ya magari. Alichafua bila kutaka mwanajeshi na akamuwashia moto. Alifariki katika eneo la tukio”, mashahidi walibaini.
Wanafahamisha kuwa waakazi wengi wakiwemo vijana wa CNDD-FDD waliingilia kati na kutaka kujichukulia sheria mikononi lakini mwanajeshi mwingine akaingilia kati.
Afisa katika FDNB ( jeshi la ulinzi wa taifa la Burundi) anayehusika na operesheni katika eneo hilo, alifahamisha kuwa muhusika wa mauwaji hayo alikamatwa.
” atahukumiwa kwa mjibu wa sheria”.
Kisa hicho kiliibua mvutano mkali kati ya mwanajeshi na wakaazi wa Nyamitanga. Nenda rudi ilisimama kwa muda wa masaa matano. Hali hiyo ilimalizika baada viongozi tawala na maafisa wa jeshi kuingilia kati.
Wakaazi wanaomba mwanajeshi huyo aliyehusika na kifo hicho ahukumiwe katika kesi ya mafumanio
You might also like
North Kivu : timid demonstration against President Macron’s arrival in the DRC
A demonstration has been organized in Goma this Thursday since the morning hours. Citizen movements and pressure groups are protesting against the arrival of French President Emmanuel Macron in the
Masisi : hofu imetanda eneo la Sake kutokana na mapigano kati ya jeshi na kundi la M23
Hali ya taharuki imeshuhudiwa alhamisi hii ndani ya jiji la Sake kwenye umbali wa takriban kilometa 20 magharibi ya mji wa Goma( makao makuu ya mkoa wa Kivu kaskazini) mashariki
Rwanda-DRC : Kigali inadai kuwa aduwi wake peke katika ukanda huu ni Kinshasa
Waziri wa Rwanda wa diplomasia alikuwa bungeni alhamisi kwa ajili ya ” kueleza” wawakilishi hao wa wananchi kuhusu hali ya sasa ya ushirikiano wa Rwanda. Daktari Vincent Biruta alihakikisha kuwa
