Buganda: kijana Imbonerakure auwawa na mwanajeshi

Buganda: kijana Imbonerakure auwawa na mwanajeshi

Kisa hicho kilitokea alhamisi hii kwenye transversale ya nne katika kijiji cha Nyamitanga mkoa wa Cibitoke (kaskazini-magharibi mwa Burundi). Mwanajeshi alimpiga risasi kijana Imbonerakure (mfuasi wa tawi la vijana la chama cha CNDD-FDD). Alifariki papo hapo. Muhusika wa mauwaji hayo alikamatwa. HABARI SOS Médias Burundi

Muathiriwa ni kijana mwanafunzi aliyekuwa akielekea kumalika masomo mwaka ujao. Kwa mjibu wa mashahidi, ilikuwa majira ya saa moja ambapo Lahay Roy Niyera aliuwawa.

” Alikuwa akijaribu kuondoa udongo katika barabara ili kuruhusu nenda rudi ya magari. Alichafua bila kutaka mwanajeshi na akamuwashia moto. Alifariki katika eneo la tukio”, mashahidi walibaini.

Wanafahamisha kuwa waakazi wengi wakiwemo vijana wa CNDD-FDD waliingilia kati na kutaka kujichukulia sheria mikononi lakini mwanajeshi mwingine akaingilia kati.

Afisa katika FDNB ( jeshi la ulinzi wa taifa la Burundi) anayehusika na operesheni katika eneo hilo, alifahamisha kuwa muhusika wa mauwaji hayo alikamatwa.

” atahukumiwa kwa mjibu wa sheria”.

Kisa hicho kiliibua mvutano mkali kati ya mwanajeshi na wakaazi wa Nyamitanga. Nenda rudi ilisimama kwa muda wa masaa matano. Hali hiyo ilimalizika baada viongozi tawala na maafisa wa jeshi kuingilia kati.

Wakaazi wanaomba mwanajeshi huyo aliyehusika na kifo hicho ahukumiwe katika kesi ya mafumanio

Previous Cibitoke: watu 15 walipatikana na ugongwa wa kipindipindu kwa kipindi cha chini ya wiki mbili eneo la Rugombo
Next Rwanda-DRC: ndege ya kivita ya Kongo kwa mara nyingine imevunja sheria na kuingia katika anga ya Rwanda