Cibitoke: watu 15 walipatikana na ugongwa wa kipindipindu kwa kipindi cha chini ya wiki mbili eneo la Rugombo

Cibitoke: watu 15 walipatikana na ugongwa wa kipindipindu kwa kipindi cha chini ya wiki mbili eneo la Rugombo

Janga la kipindipindu linaripotiwa katika eneo la Mparambo tarafani Rugombo mkoa wa Cibitoke (kaskazini magharibi mwa Burundi) tangu wiki mbili zilizopita. Wagonjwa 15 walipatikana. Ukosefu wa maja safi ndio chanzo cha ugonjwa huo. Maafisa wa afya katika mkoa wa Cibitoke wanafahamisha kuwa hawajuwi ulikotoka ugonjwa huo. HABARI SOS Médias Burundi

Visa vya maradhi ya kipindipindu vinaripotiwa mnamo siku chache zilizopita katika eneo la mkoa wa Cibitoke kwenye mwambao wa mto wa Rusizi, unatofautisha nchi za Burundi na DRC. Angalau watu 15 waliopatikana na ugonjwa huo walipokelewa katika huduma ya dharura ya kituo cha afya cha Rugombo.

Wagonjwa wote kulingana na vyanzo katika utawala wanatoka katika kijiji cha Mparambo I tarafani Rugombo kwenye umbali wa kilometa kumi kutoka makao makuu ya mkoa.

Shirika la waganga wa msalaba mwekundu ambalo linatoa huduma zote lilikabidhi pia kituo hicho cha afya gari la wagonjwa kwa ajili ya kurahisisha usafiri wa wagonjwa.

Shirika la msalaba mwekundu la Burundi na kikosi cha polisi cha kukinga majanga wanawajibika kwa kasi kunyunyizia dawa ndani ya majumba ambako wagonjwa wanaishi. Nyumba zote katika eneo hilo zimepewa huduma ya maji safi.

Regideso ( mamlaka ya umaa ya maji na umeme) inashiriki pia ili maji safi yapatikane. Eneo lililoathiriwa linakabiliwa na ukosefu wa huduma hiyo.

Viongozi wa afya mkoani Cibitoke wanafahamisha kuwa kampeni ya kuwahamasisha raia imeanza kwa ushirikiano na viongozi tawala.

” ni kutokana na uhaba wa maji safi ambapo ugonjwa huo uliripuka”, wanasema.

Previous Cibitoke: 15 people affected with cholera in less than two weeks in Rugombo
Next Buganda: kijana Imbonerakure auwawa na mwanajeshi

About author

You might also like

Human Rights

Rumonge: a child killed and two others injured in torrential rains

The province of Rumonge’s capital (south-west of Burundi) counted one death, two injuries and a dozen houses destroyed following torrential rains. A report shared by the administrative authorities who request

Society

Bubanza : farmers complain about the lack of corn seeds

The provincial office of agriculture and livestock in Bubanza province (western Burundi) received corn seeds imported from Zambia. Less than 30 tons of seeds were received, an insignificant quantity compared

Economy

Kirundo-Muyinga : fuel theft from vehicles rages

As the fuel shortage has reached its peak, criminals are organizing themselves to empty vehicle tanks at night.This situation is reported in Muyinga and Kirundo (north-eastern Burundi). Kirundo where mob