Rwanda-DRC: ndege ya kivita ya Kongo kwa mara nyingine imevunja sheria na kuingia katika anga ya Rwanda

Rwanda-DRC: ndege ya kivita ya Kongo kwa mara nyingine imevunja sheria na kuingia katika anga ya Rwanda

Serikali ya Rwanda ilifahamisha kuwa anga yake imeingiliwa na ndege la kivita ya DRC(Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo). Viongozi wa Rwanda wamekitaja kisa hicho kama ” cha uchokozi” kinachokiuka makubaliano ya Luanda na Nairobi. HABARI SOS Médias Burundi

Kulingana na tangazo, tukio hilo lilijiri majira ya saa sita mchana jumatano hii tarehe 28 disemba 2022. Ni kwenye mwambao wa ziwa Kivu kati ya nchi hizo mbili jirani za kanda ya maziwa makuu ya afrika kulingana na viongozi wa Rwanda.

” Kisa hicho kinaorodheshwa katika mlolongo wa visa vya uchokozi kikiwemo kisa cha cha ndege ya kivita iliyotuwa kwenye uwanja wa Rubavu (mkoa wa magharibi mwa Rwanda) tarehe 7 novemba 2022″ , Rwanda inafahamisha na kukumbusha pia kwamba ” viongozi wa Kongo walikubali kisa hicho” baada ya kupinga katika mwezi wa novemba.

” Visa hivyo vya uvamizi vinavyorudia vinakwenda kinyume na makubaliano na mchakato wa amani ya Luanda na Nairobi” , yanasomeka ndani ya tangazo.

Na kushambulia kuwa ” viongozi wa DRC wanaonekana kutiwa moyo na motisha ya baadhi ya wajumbe wa jamii ya kimataifa wanaotuhumu kwa mara kadhaa nchi ya Rwanda makosa ya aina yote nchini DRC na kupuuza ukiukwaji wa DRC”.

Kulingana na serikali ya Rwanda, uchokozi huo inatakiwa
“kusimama “.

Serikali ya kongo halijatoa maelezo kuhusu madai hayo mapya. Chumba chetu cha habari kimejaribu kuwasiliana na wizara ya Kongo ya mawasiliano na msemaji wa serikali bila mafanikio.

Uhusiano unazidi kuzorota kati ya mataifa hayo mawili ya maziwa makuu ya afrika kutokana na mzozo mashariki mwa nchi hiyo kubwa ya afrika ya kati ambapo kundi la M23, kundi la silaha la Kabila la watutsi linazidi kudhibiti maeneo, rais Félix Tshisekedi yeye binafsi akituhumu Rwanda kuunga mkono kundi hilo.

Lakini ijumaa iliyopita, kundi la M23 liliachia sehemu ya ngome zake kwa kikosi cha jumuiya ya afrika mashariki. Ni ngome zinazopatikana katika wilaya ya Nyiragongo mkoa wa Kivu kaskazini ( mashariki mwa DRC).

Kundi hilo la waasi lilifahamisha kuwa ” linataka kuonyesha nia yake ya kuchangia katika amani ya kudumu”. Ni baada ya kikao cha Luanda (Angola) na awamu ya tatu ya mazungumzo ya Nairobi (Kenya) kuhusu kumaliza mzozo mashariki mwa Kongo. Kundi la M23 hata hivyo lilifahamisha ” litajipa haki za kuwahami wananchi wasiokuwa na hatia iwapo watauwawa”.

Hivi karibuni, mashirika ya kimataifa mengi, nchi na wataalam wa UN waliunga mkono tuhuma za viongozi wa Kongo dhidi ya Rwanda. Madai ambayo serikali ya Rwanda inaendelea kutupia mbali.

Upande wake, Rwanda inatuhumu FARDC ( jeshi la Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo) kushirikiana na kundi la FDLR kwa lengo la kuvuruga ardhi yake.

Kundi la M23 kundi la waasi la zamani lililochukuwa tena silaha mwishoni mwa mwaka wa 2021, linatuhumu viongozi wa Kongo kutotekeleza ahadi zake za kuwarejesha katika maisha ya kawaida wapiganaji wake.

Uwanjani, ma kumi ya ya mia ya raia walitoroka maeneo yao kwa ajili ya kutafuta hifadhi katika maeneo salama ou nchini Uganda.

Tangu mwanzoni mwa mwezi juni mwaka huu, kundi hilo la M23 lilidhibiti maeneo mengi ya mkoa wa Kivu kaskazini likiwemo la Bunagana mjini wa mpakani na Uganda.

Siku chache zilizopita, viongozi wa Kongo walituhumu kundi la M23 kuwauwa wananchi 272 katika vijiji viwili chini ya udhibiti wake, UN ikisema ni watu 130 waliouwawa. Waziri wa Kongo ya sheria alipeleka mashtaka mbele ya ICC (mahakama ya uhalifu ya kimataifa).

Kundi la M23 lilitupilia mbali mashtaka hayo na kuomba uchunguzi huru ufanyike.

Previous Buganda: kijana Imbonerakure auwawa na mwanajeshi
Next Mutaho: the post office manager killed