Bubanza : Familia mia tano walionyanganywa ardhi yao wanaomba kupewa makaazi mengine

Bubanza : Familia mia tano walionyanganywa ardhi yao wanaomba kupewa makaazi mengine

Zaidi ya watu 200 wamejielekeza mbele ya ofisi ya gavana wa mkoa wa Bubanza (Magharibi mwa Burundi) jumatatu hii na kuandamana kwa mchana wote.Walimuomba gavana kuwatetea. Walinyanganywa ardhi kama zaidi ya wakaazi wengine 7800 ambao maeneo yao palijengwa kambi ya kijeshi ya Mudubugu. Utawala uliwakubalia kuhamishiwa katika mkoa wa Rutana (kusini-mashariki mwa Burundi). Zoezi hilo halikufanyika. Familia nne zilikimbilia nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo wakati ambapo sita zingine walielekea katika maeneo mengine ya nchi. Familia hizo zinakimbia njaa sababu hawakulima. HABARI SOS Medias Burundi

Familia zote zilizokuwa na ardhi karibu na kambi ya Mudubugu hawana haki ya kutumia ardhi yao tangu mwezi agosti mwaka huu.

Viongozi wa kambi walichukuwa eneo la heka 1069. Wamiliki hawakupewa fidia.

“Mimi ni mjane tangu miaka 23 iliyopita. Mume wangu aliniweka ndani ya hii ardhi.Nilikuwa nafanya kilimo hapa hadi wanajeshi waliponizuia. Hichi ndicho kitega uchumi. Tuko katika hatari ya kufa na njaa mimi na familia yangu iwapo hawataturuhusu tena,” alibaini Jeanette.

Zaidi ya watu 200 walijielekeza kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa wa Bubanza ili kumtaka gavana awafanyie utetezi.

Kwa jumla familia 5000 zenye wajumbe zaidi ya 8000 hawana haki tena kwenye mashamba yao. Hawana hata haki ya kuvuna.

“Tunataka watuwache tuendelee kulima hadi pale idara zinazohusika zitaweka wazi na kusema Nani mmiliki wa ardhi hii”, alisema Pascal.

Kambi ya Mudubugu inapatikana katika ardhi zilizo ndani ya tarafa tatu.Tarafa ya Gihanga na Bubanza (mkoa wa Bubanza Magharibi) na Buganda (mkoa wa Cibitoke kaskazini-magharibi mwa Burundi) na ardhi yake inajumulisha vijiji saba.

Kambi hiyo ina sehemu ya kufanyia mazoezi ya kupiga risasi pamoja na eneo la kuripua vifaa vilivyoharibika.

Miaka ya 1980, wakaazi wa maeneo ya karibu walipewa fidia kutokana na madhara yaliyotokea na kuahidiwa kuwa watahamishwa mahala pengine.

” Walitukubalia mashamba eneo la Gihofi tarafani Bukemba mkoa wa Rutana. Lakini hawakuwahi kutekeleza ahadi hiyo” alifafanua mkaazi.

Wamiliki waliruhusiwa kuendelea kutumia ardhi yao isipokuwa tu katika kipindi cha mazoezi ya kupiga risasi na kuripua vifaa vya jeshi ili kukinga ajali.

Athari zinashuhudiwa

Familia sita tayari walikimbia eneo la Mudubugu, baadhi walitoa mabati kwenye nyumba zao. Wengine walikimbilia nchini DRC.

” Wanafunzi hawaendi sheleni. Kuna hata mwanaume aliyekufa kutokana na njaa.Watoto wanaomba omba karibu na kambi. Ni hali ya kusikitisha, ” kwa mjibu wa mkaazi mmoja wa eneo la Mudubugu.

Gavana wa mkoa wa Bubanza aliahidi kufuatilia kwa karibu kesi hiyo. Faili hiyo iliwasilishwa kwenye ofisi ya mpatanishi ambaye aliwahi kufika eneo hilo.

Ni kisa cha pili cha familia nyingi kunyimwa haki kwenye ardhi yao katika mkoa wa Bubanza baada ya kisa cha eneo la Muzinda tarafani Rugazi ambapo familia zilifukuzwa nje ya ardhi yao pasina kupewa fidia

Previous Bubanza: five thousand households expropriated ask to be relocated
Next Mugamba: a retired policeman died in obscure circumstances