Mwanamfalme Louis Rwagasore: Hospitali inayoumwa zaidi ya wagonjwa inayowapokea

Mwanamfalme Louis Rwagasore: Hospitali inayoumwa zaidi ya wagonjwa inayowapokea

Tangu kuanzishwa mwaka 1945, cliniki ya Prince Louis Rwagasore ilitoa huduma kwa wagonjwa mashuhuri na watu wa kipato cha juu wa wakati wa ukoloni na baadaye. Ilipendwa na kuendelea kupendwa kutokana na mfumo wake wa ujenzi wa kikoloni lakini jengo hilo limechakarika na liko katika hatari ya kubomoka kutokana na kutoshughulikiwa. HABARI ya SOS Medias Burundi

Kliniki ya Prince Louis Rwagasore iliyojengwa kati kati mwa jiji la Bujumbura makao makuu ya kiuchumi, sasa ni jengo lililochakarika. Ni kituo cha afya cha watu wenye kipato cha chini waliothubutu kwenda kutafuta huduma zinazolingana na uwezo wao mdogo.

Kituo hicho cha afya hakiaminiki. Watu wanakwenda kujitibisha lakini kwa maoni ya wagonjwa wenye uelewa, ni rahisi sana kupata kifo.

Manesi kwenye hospitali hiyo ya zamani kabisa ndani ya nchi ndogo ya afrika mashariki wanasema hakuna kinachoendelea.

“Tuko na tatizo la dawa. Kutokana na uhaba wa dawa, hatuwezi kutoa huduma hasa katika kipindi hichi cha majanga. Kuna tatizo ya vifaa : Kwenye maabara, chumba cha upasuaji, ndani ya huduma zote. Vifaa vimeharibika. Tunashudia mara kwa mara matatizo” alisema nesi mmoja aliyefanya miaka 29 ya kazi kwenye kliniki ya Prince Louis Rwagasore.

“Kuhusu hospitali hiyo, tuna matatizo kabisa. Mara nyingi unaweza kuwa na afya nzuri, lakini unapokwenda kwenye kliniki ya Prince Louis Rwagasore, utapata maradhi. Vyote vimechafuka, vyoo ….mbu wanakung’ata”, anahakikisha Hervé mgonjwa aliyekutwa kwenye mapokezi.

Kama aliyeshuhudia mmoja kati ya ma ripoti wetu, panya wanakula michafu ya hospitali hiyo iliyowekwa ndani ya ndoo ambazo ziko wazi.

“Tuna matatizo ya kihistoria ya uhaba wa wafanyakazi, madaktari bingwa na madawa na isitoshi kuna rushwa na matumizi mabaya ya bajeti. Huduma za afya zinakabiliwa na matatizo kwa kipindi cha miaka tisa hadi sasa.” alibaini mganga wa magonjwa ya wanawake kwenye hospitali hiyo ambaye hakutaka jina lake litambulike.

Kwa mjibu wa mganga mkuu wa kliniki hiyo jawabu liko katika mikono la serikali.

“Ili huduma za hospitali ziendeshwe, ni lazima bajeti ipatikane. Ni miaka mingi tukiomba bajeti kwa serikali ili tuendeshe hospitali hiyo ya umaa lakini tunapata moja kwa kumi tunazoomba, ni kawaida huduma za hospitali kutokuwa vizuri” alifahamisha Dk Bonith Havyarimana mganga mkuu wa kliniki ya Prince Louis Rwagasore.

Previous Prince Louis Rwagasore: a hospital as sick as the patients it receives
Next Bujumbura : singer Olègue is free