Karusi-Rumonge: mikoa hiyo imewapata magavana wapya

Karusi-Rumonge: mikoa hiyo imewapata magavana wapya

Léonard Niyonsaba na Dévote Nizigiyimana, wa kwanza ni gavana mpya wa mkoa wa Rumonge (Kusini-magharibi mwa Burundi) na mwingine ni gavana wa mkoa wa Karusi (Mashariki ya kati mwa Burundi). Waliidhinishwa na baraza la seneti siku ya jumatano baada ya majina yao kupendelezwa na rais wa jamuhuri. Wakaazi wa mkoa wa Rumonge wanasema kuridhishwa na mabadiliko hayo ya kiongozi wa mkoa. Gavana huyo anayeondoka ameacha mkoa huo ukiwa masikini licha ya fursa nyingi zilizopo, ikiwa ya mwisho nchini katika rikodi ya elimu na kwingine. Wakaazi wa mkoa huo wanaomba kiongozi mpya kuunganisha wananchi waliotenganisha wa gavana aliyesimamishwa. HABARI SOS Médias Burundi

Léonard Niyonsaba ambaye ameteuliwa kuwa gavana mpya wa mkoa wa Rumonge, hadi sasa alikuwa mkuu wa itifaki katika ofisi ya gavana aliyeachishwa ngazi Consolateur Nitunga. Huyu naye aliteuliwa kuwa mshahuri wa pili kwenye ubalozi wa Burundi nchini DRC.

Mkoa mwingine uliopata kiongozi mpya ni Karusi. Ni Dévote Nizigiyimana. Yeye alikuwa mfanyakazi kwenye ENS ( Chuo cha waalimu).

Mkoani Rumonge, wakaazi wanalaani kuona Consolateur Nitunga ameacha mkoa ambao haujaweza kunufaika na fursa zilizopo katika mkoa huo.

” Alijulikana katika visa vya rushwa kuliko kupendelea mzunguko wa biashara. Hatua ya kuruhusu bidhaa za nafaka kuingia tena nchini Burundi haikuleta matunda. Bei ya kilo moja ya mchele ni hadi 3600 sarafu za Burundi kwa mfano wakati ambapo tuko na bandari ambako kunapita bidhaa kwa urahisi, [….], wanalalamika wakaazi huku wakikumbusha kuwa rais Ndayishimiye alimuaibisha gavana huyo aliyeondolewa katika mwezi juni kutokana na visa vya ulaji rushwa kuhusu mafuta ya gari na theluji. Kuna mshahuri ya gavana wa mkoa wa Rumonge aliyefutwa kazi kwa hoja hizo hizo mwezi huu.
Waangalizi maeneo hayo wanahofu kuwa gavana mpya atakuwa na kibarua kigumu cha kuunganisha wananchi waliotofautishwa na mtangulizi wake sababu ” alifanya kile chote anachoweza ili kutofautisha watu kwa misingi ya ukabila. Ana ukabila mwingi na chuki dhidi ya Watutsi na wapinzani wote wa kisiasa”.
Rumonge ni kati ya mikoa ambayo iko na fursa nyingi. Mkoa huo unapatikana kwenye mwambao wa ziwa Tanganyika na unazalisha kwa wingi Mafuta ya migazi inayotumiwa katika nchi hii ndogo ya afrika mashariki na nchi jirani pamoja pia uzalishaji wa matunda.

Previous Karusi-Rumonge: the two provinces have new governors
Next Uvira: watu sita akiwemo askali jeshi wauwawa katika mapigano kati ya jeshi na kundi la Maï Maï