Uvira: watu sita akiwemo askali jeshi wauwawa katika mapigano kati ya jeshi na kundi la Maï Maï

Uvira: watu sita akiwemo askali jeshi wauwawa katika mapigano kati ya jeshi na kundi la Maï Maï

Wananchi wawili, waasi watatu na askali jeshi mmoja waliuwawa siku ya alhamisi kwenye eneo la Mubere. Ni katika mji wa Kigoma wilaya ya Uvira ndani ya mkoa wa Kivu ya kusini mashariki mwa DRC. Walifariki dunia katika mapigano kati ya FARDC (jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo) na makundi ya Mai Maï Kijangala. HABARI SOS Médias Burundi

Mbali na watu hao waliouwawa, na wengine kujeruhiwa, wakaazi wanaendelea kuyatoroka maeneo yao kwa ajili ya usalama wao. Wamepewa hifadhi eneo la Sange (daima katika mkoa wa Kivu ya kusini).

Kwa mjibu wa vyanzo vya ndani, milio ya silaha nzito na za kawaida ilisikika.

“Mchungaji wa kanisa mmoja na mwanamke aliyekuwa pamoja naye, walijeruhiwa na vipande vya bomu, alisema mkaazi mmoja.
Kulingana na mashahidi, waasi wa Maï Maï Kijangala walichoma moto angalau nyuma 12.
Mashirika ya kiraia katika bonde la Rusizi wanathibitisha kuwa wakaazi wa maeneo ya vijiji vya Mubere Nakihima na Kabere ambapo mapigano yalifanyika wanaendelea kutoroka maeneo yao na kuelekea maeneo ya Sange na Kigoma.

“Tulimpoteza mwanajeshi mmoja na mwingine kujeruhiwa”, alitoa ushuhuda mwanajeshi wa kikosi ca 3304 ambaye jina lake lilihifadhiwa.

Na kuendelea “Tuliwauwa waasi watatu wa Maï Maï akiwemo mmoja mwenye asili ya burundi aliyefahamika kwa jina maarufu Kibonge”.

Kundi la Maï Maï Kijangala linashirikiana na kundi la vijana wafuasi wa chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD (Imbonerakure), kwa mjibu wa vyanzo vya ndani katika mkoa wa Kivu ya kusini.

Kulingana na vyanzo vingi, wanasaidia katika kuelekeza jeshi la FDNB (jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo) ili kutafuta makundi ya silaha ya Burundi yaliyopiga katika mkoa wa Kivu ya kusini, hasa kundi la Red-Tabara linalochukuliwa na viongozi wa Burundi kama kundi la kigaidi.

Previous Karusi-Rumonge: mikoa hiyo imewapata magavana wapya
Next Karusi: threats of arrest weigh on seven opponents