Giharo: mjumbe wa chama cha CNDD-FDD mwenye ushawishi anazuiliwa jela

Giharo: mjumbe wa chama cha CNDD-FDD mwenye ushawishi anazuiliwa jela

Nestor Butisi, mjumbe wa chama tawala tarafani Giharo mkoa wa Rutana (Kusini mashariki mwa Burundi) amesimamishwa jumatatu iliyopita. Anatuhumiwa kufanya biashara haramu ya mbolea na kutengeneza pombe haramu. Anazuiliwa katika gereza la mkoa. HABARI SOS Médias Burundi

Kulingana na wakaazi wa tarafa ya Giharo, ni polisi waliomusimamisha baada ya msako kufanyika nyumbani kwako.

Polisi iligundua nyumbani kwake mifuko 35 ya mbolea ya kizungu, mifuko 17 ya sukari na jerikani 9 za pombe iliyopigwa marufuku.

Mfuasi huyo wa chama cha CNDD-FDD mwenye ushawishi alishikiliwa katika gereza la kamishena ya polisi tarafa Giharo kwa masaa 24.

Alichukuliwa na Mwendeshamashtaka wa jamuhuri mkoani Rutana siku moja baada ya kukamatwa na kutumwa katika gereza la mkoa alhamisi iliyopita nyakati za alasiri.
Vyanzo katika chama tawala vinasema kuwa katibu mkuu wa chama cha CNDD-FDD tarafani Giharo alifanikiwa kumuelewesha mwendeshamashtaka ili kesi isiwe ya mafumanio kwa kosa ” biashara haramu ya mbolea ” sawa na matakwa ya serikali kuhusiana na kupiga vita biashara haramu ya mbolea.
Fundi wa kilimo mmoja pia mfuasi wa chama tawala alisimamishwa mwaka jana kwa tuhuma za wizi wa tani nyingi za mbolea. Hakumaliza muda mrefu katika gereza la korti ya Rutana. Aliachiliwa kwa ushawishi wa kiongozi wa chama cha CNDD-FDD.
Bwana Butisi alitajwa katika visa vingi vya kuwahujumu wapinzani mkoani Rutana ikiwa ni pamoja na visa vya kukamatwa kinyume cha sheria.

Previous Photo of the week: villages are emptying of their populations in North Kivu
Next Karusi: three CNDD-FDD party members in detention after discovery of weapons