DRC-Rwanda: Uganda imetuhumiwa kwa kiwango sawa na Rwanda

DRC-Rwanda: Uganda imetuhumiwa kwa kiwango sawa na Rwanda

Ma mia ya watu jumatatu hii waliandamana mjini Goma makao makuu ya mkoa wa kivu-kaskazini mashariki mwa DRC.
Wanazituhumu nchi za Rwanda na Uganda kufanya unafiki katika mgogoro kati ya DRC na kundi la silaha la M23.
Wanaomba jamii ya kimataifa kuingilia kati. Viongozi wa kijeshi waliwasihi wanaoandaa sherehe kama hizo kuacha wakihofia maaduwi kupenyeza. HABARI SOS Médias Burundi

Mandamano hayo yaliandaliwa na mashirika ya kiraia ya mkoa wa kivu ya kaskazini na viongozi wa PNC (Sera ya kitaifa ya raia wa Kongo). Wanalaani maeneo mengi ya wilaya ya Rutshuru kudhibitiwa na kundi la silaha la M23.

“Wandamanaji walielekea kwenye mpaka wa Kongo na Rwanda katika eneo maarufu ‘grande barrière’ wakionyesha mandishi yanayowatuhumu marais wa Rwanda na Uganda kuwa wanafiki” mashahidi wanasema.

Katika matamshi yao, wandamanaji waliomba ushirikiano wa kitaifa na kimataifa ili kumaliza tatizo la usalama mdogo kutokana na kudhibitiwa kwa maeneo mengi na kundi la M23 katika wilaya ya Rutshuru na mji wa Bunagana karibu na mpaka wa Uganda.

” Tunataka kuonyesha ulimwengu uzembe wa jamii ya kimataifa ambayo inaangalia pasina kuwajibika namna nchi yetu inavyovamiwa na Rwanda na Uganda. Lakini pia ni fursa kwetu ili kuunga mkono kwa njia moja ama nyingine jeshi la FARDC ( Jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo) ambalo liko uwanjani dhidi ya kundi la M23. Tunataka kuanzisha jamii kubwa nyuma ya jeshi” walifahamisha walioandaa mandamano hayo ambao walihakikisha kuwa walikuwa na mpango wa kuvuka mpaka na kuingia kwenye ardhi ya Rwanda, jambo ambalo vikosi vya usalama na ulinzi vilizuia.

” Tunaomba raia wa jamuhuri ya Kongo kuweka wazi makubaliano aliyosaini na Rwanda ” alieleza kwa hasira mjumbe wa shirika kwa ajili ya mabadiliko ( Lucha)” .

Katika mandamano hayo, baadhi ya wandamanaji waliwaomba viongozi wa kijeshi kuwapa mafuko ya kijeshi ili kusaidia wanajeshi kwenye uwanja wa mapambano ili kulinda taifa.

mashirika ya kiraia yanaomba wananchi ” Kupigania uhuru wao ” yakidai kuwa hakuna anayeweza kukukomboa mbali na wewe binafsi “.
” Tuko hapa ili kulinda nchi yetu. Tunatakiwa kupigana ili tuhakikishe nchi kuwa ardhi yetu imetoka katika mikono ya adui. ” alifahamisha Mambo Kawaya kiongozi wa mashirika ya kiraia ya Nyiragongo ( eneo jirani la Rutshuru).

Katika mandamano hayo, makundi ya vijana walifungua na kupora ndani ya vibanda vinavyomilikiwa na watu wanaotumia lugha ya Kinyarwanda. Polisi iliingilia kati haraka.
Lakini mjumbe mmoja wa jamii ya Banyamulenge alisimamishwa jumatatu kwenye uwanja wa ndege wa Goma. Louis Nkumbuyinka alilengwa kutokana na kabila lake la Tutsi, kwa mjibu wa vyanzo vyetu.

Katika tangazo la siku ya jumatatu, gavana mwanajeshi wa mkoa wa Kivu-kaskazini luteni jemedali Ndima Kongba Constant anawaomba walioandaa mandamano kuyaacha akisisitiza kuwa kisa kama hicho kinaweza kuwasaidia maaduwi kujipenyeza”.

Mazungumzo kuahirishwa.

Awamu ya tatu ya mazungumzo ya amani na usalama nchini DRC yaliahirishwa 21-27 novemba.

Ofisi ya mpatanishi kuhusu amani na usalama mashariki mwa DRC ilisogeza mbele kwa kipindi cha wiki mbili awamu ya tatu ya mazungumzo kati ya raia wa Kongo ambayo awali yalipangwa kufanyika tarehe 7-14 novemba mjini Nairobi, mji mkuu wa Kenya.

Katika kipindi hicho cha mwanzo, mpatanishi atakuwa katika mazungumzo kuhusu tabia nchi nchini Misri.

Katika tangazo, ofisi ya raia Uhuru Kenyata, rais mstaafu wa Kenya anayeendesha mazungumzo hayo ambayo yanafahamika kama mchakato wa Nairobi, na upande wa Kongo hawatapatikana katika kipindi cha awali walichokuwa wameahidiana.

” Mjumbe maluum wa DRC kwa ajili ya mchakato wa Nairobi atasafiri kuhudhuria mazungumzo kwenye baraza la usalama la umoja wa mataifa mjini New York. Wakati huo huo, mpatanishi wa EAC ( jumuiya ya afrika mashariki) katika mchakato wa Nairobi atashiriki mazungumzo kuhusu tabia nchi ya COP27 nchini Misri kama mwenyekiti wa kamati ya UA(Umoja wa afrika) kuhusu mabadiliko ya tabia nchi” linafahamisha tangazo.
Mchakato unaendelea kati ya makundi ya waasi na serikali ya Kongo pasina kushirikisha kundi la machi 23 (M23) ambalo linasonga mbele kwenye uwanja.

Kundi hilo linaloundwa kwa sehemu kubwa na watu wa kabila la watutsi wenye asili ya Kongo lilibaguliwa kwenye mazungumzo na viongozi wa Kongo ambao wanalitaja kama ” kundi la kigaidi”.

Rais wa Rwanda anayetuhumiwa bila ushahidi na mwenzake wa Kongo kusaidia waasi, aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter siku ya jumatatu kuwa mchakato wa Luanda (Angola) na Nairobi (Kenya ) na juhudi zingine za kimataifa zimesalia njia peke za kupata suhulu ya mgogoro unaoendelea mashariki mwa nchi hiyo kubwa ya afrika ya kati.

” Tunatakiwa kukubaliana na kutekeleza ” aliandika

Hata kama mashirika ya kiraia na makundi mengine ya shinikizo yameanza kuhusisha Uganda, viongozi wa Kongo bado wako makini kuhusiana na hilo ingawa mnamo miezi michache ilizopita waliwahi kulaumu kuwa mtoto wa rais wa Uganda jemedali Muhoozi Kainerugaba aliyesimamishwa kwenye wadhifa wa kamanda wa kikosi cha ardhini baada ya kuandika kwenye Twitter ” Mimi na mjomba wangu Kagame tutakwenda nchini DRC ili kutokomeza na kushinda kundi la waliofanya mauwaji ya halaiki FDLR “.

Uganda ina wanajeshi kwenye ardhi ya Kongo katika ushirikiano wa nchi hizo mbili kwa lengo la kupigana dhidi ya kundi la ADF linalopigana na serikali ya Uganda na ambalo linachukuliwa la kanda, marekani na umoja wa mataifa kama” kundi la kigaidi”.

Previous DRC-Rwanda: Uganda indexed at the same time as Rwanda
Next Bujumbura: a student loses his left eye in a caning session