Cibitoke: zaidi ya vitenge 300 vilikamatwa kwa mfuasi wa CNDD-FDD eneo la Buganda
Zaidi ya vitenge 300 kutoka jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo vilikamatwa na polisi kwa mfuasi wa chama tawala mwenye ushawishi. Msako ulifanyika eneo la Nyamitanga kijiji cha Ndava tarafani Buganda (mkoa wa Cibitoke kaskazini magharibi mwa Burundi). Ilikuwa tarehe 25 oktoba.Wakaazi wanaomba sheria itumike. Idara ya sheria mkoani Cibitoke inafahamisha kuwa taarifa imewafikia na kuzidi kuwa uchunguzi umeanzishwa. HABARI SOS Médias Burundi
Kwa jumla vitenge 322 vilikamatwa jumanne tarehe 25 kwake Adeline Ingabire mjumbe wa baraza la tarafa ya Buganda ambaye ni kutoka chama tawala na yuko kwenye orodha ya wabunge waliochaguliwa katika mkoa wa Cibitoke.
Mke huyo wa mshahuri wa zamani wa balozi wa Burundi mjini Brussels ni mmoja kati ya viongozi wakuu wa chama cha CNDD-FDD. Anajulikana kama mwanamke mwenye ushawishi ndani ya chama tawala.
” Sio kisa cha kwanza. Alituhumiwa mara nyingi kuhusika na biashara haramu hasa biashara ya vitenge”, chanzo katika polisi kwenye makao makuu ya mkoa wa Cibitoke kilieleza.
Mwanamke huyo aliwahi kuitishwa katika mwaka wa 2021 bila hata hivyo kusikitika wakati akijaribu kuingiza nchini Burundi bidhaa ya vitenge pasina kulipa ushuru kwenye mamlaka ya ushuru na kodi OBR nchini kupitia mpaka kati ya Burundi na Kongo kwenye mto Rusizi.
Mfanyabiashara mmoja anahakikisha kuwa mtuhumiwa huyo alinufaika kwa kipindi kirefu na ushirikiano wa vigogo wa chama tawala.Anazidi kuwa mtuhumiwa huyo hataguswa.
“Maajabu zaidi, vitenge hivyo vitarudishwa kwake haraka wakati ambapo vimekamatwa na OBR,” analalamika mfanyabiashara huyo.
Habari hiyo inathibitishwa na polisi ya Cibitoke ambayo inazidi kuwa vitenge hivyo vilikabidhiwa vyombo vya sheria.
Akiulizwa juu ya mkasa huo, Mwendeshamashtaka wa jamuhuri mkoani Cibitoke amefahamisha kuwa uchunguzi umeanzishwa. Anaomba watu kusubiri kwa utulivu matokeo ya uchunguzi huo.
Amejizuia kusema lolote kuhusiana na swala la kwa nini mtuhumiwa hakusimamishwa wakati alifumaniwa na biashara haramu.