Rutana: mfuasi mwenye ushawishi wa chama cha CNDD-FDD akungwa mwaka mmoja jela

Rutana: mfuasi mwenye ushawishi wa chama cha CNDD-FDD akungwa mwaka mmoja jela

Nestor Butisi Nibigira mfanyabiashara na mfuasi mwenye ushawishi wa chama cha CNDD-FDD tarafani Giharo amekatiwa kifungo cha mwaka mmoja jela. Atalazimika kulipa faini ya milioni 2.5 sarafu za burundi. Uamzi umechukuliwa jumatano hii alasiri baada ya kesi dhidi yake asubuhi ya hiyo siku katika korti ya Rutana (Kusini mashariki mwa Burundi). HABARI SOS Médias Burundi

Mtuhumiwa aliripoti mbele ya jopo la majaji wa korti ya mkoa wa Rutana jumatatu ambalo limeamuru asalie gerezani.

” Kesi dhidi yake, iliharakishwa zaidi ya kesi za wafungwa wengine”, chanzo kwenye korti ya Rutana kinahakikisha.

Katika siku mbili peke, aliripoti mbele ya jopo la majaji na kesi yake kusikilizwa. Maanuzi yalichukuliwa siku hiyo hiyo.

“Vigogo wa chama cha CNDD-FDD waliwashawishi majaji , waliwapa maelekezo ” , chanzo karibu na faili hiyo kinaeleza.

Nestor Butisi Nibigira alikuwa alisimamishwa na polisi baada ya msako wa tarehe 24 oktoba. Mifuko 35 ya mbolea ya kizungu, 17 ya sukari na jerikani 9 za pombe haramu vilikamatwa kwenye duka lake na nyumbani kwake.

Mfuasi huyo na mwenye ushawishi wa chama tawala anafahamika katika tarafa ya Giharo kama mtu aliyeshiriki katika kamata kamata ya kiholela ya wa upinzani hasa wafuasi wa chama cha CNL.
Kosa peke la ubadilifu na biashara haramu ndilo lilizingatiwa dhidi yake.

Previous Cibitoke: zaidi ya vitenge 300 vilikamatwa kwa mfuasi wa CNDD-FDD eneo la Buganda
Next Rutana: an influential CNDD-FDD activist sentenced to one year in prison